Baadhi ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari
ya Malindi Zanzibar yakisubiri kuhisabiwa kupata idadi kamali na thamani yake na
uzito kwa ujumla.
Zoezi likiendelea kupekuwa makunia ya Makombe ya Pwani
kutowa magunia yaliohifadhiwa Pembe za Tembo
Askari wa jeshi la Polisi wakitowa Pembe za Tembo
katika makunia wakati wa zoezi hilo leo asubuhi katika bandari ya Malindi
Zanzibar.
Zikipimwa uzito kujuwa uzito wake kila gunia likipimwa
kupata uzito wake wote.
Operesheni Ikiendelea kuhesabu Pembe za Tembo
zilizokamatwa katika bandari ya Zanzibar wakiweka hesabu sawa kuhakikisha hesabu
iliokamilika na kupata thamani yake halithi.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar
akiongoza Operesheni wa kukagua magunia yaliokuwa na Pembe za Tembo yaliokamatwa
katika bandari hiyo leo yakiwa katika harakati ya kusafirishwa nje ya Nchi
kupitia bandari hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi la Polisi Bandari
Kikosi cha KMKM, yalikuwa katika Kontena la futi 40.
Magunia haya yakiwa na sehena na makombe ya pwani
wakati katikati yakiwa na viroba vya mPembe za Tembo ambayo yakiwa yamehifadhiwa
katika Kontena likiwa tayari kusafirishwa nje ya Nchi, limegunduliwa katika
bandari ya Zanzibar jana asubuhi
Shehena kubwa ya pembe za tembo ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915 ambayo haijawahi kukamatwa nchini imenaswa katika bandari ya Zanzibar huku ikishuhudiwa na mawaziri wa serikali zote mbili wakiongozwa na waziri wa mali asili na utalii Mhe Khamis Kagasheki.
0 comments:
Post a Comment