SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, November 13, 2013

TIGO REACH FOR CHANGE KUWASAIDIA WATOTO NCHINI TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez, akizungumza na Waandishi wa Habari katika uzinduzi wa programu maalum ya ‘Reach for Change’ ambapo watanzania watatu wenye wazo bora yakuwasaidia watoto watapata fursa yakujishindia dola 25,000 kila mwaka kwa muda wa miaka mitatu ili kuendesha miradi yao.
Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo Bi. Woinde Shisael akitoa maelezo zaidi kuhusu programu maalum ya ‘Reach for Change’ inayowawezesha wajasirialamali jamii kutekeleza miradi yao yakuwasaidia watoto.
Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez, aliyesisitiza Watanzania kujitokeza kwa wingi kuandika miradi ambayo yatalenga kupata haki na kuinua ubora wa maisha ya watoto nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Reach for Change nchini Tanzania na Rwanda, Richard Gorvett, akizungumza na Waandishi wa Habari. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez, akifuatiwa na Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo Bi. Woinde Shisael.

0 comments:

Post a Comment