SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, November 12, 2013

TANZANIA HORTICULTURE ASSOCIATION (TAHA) YATOA SOMO KWA VIONGOZI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro  ambaye alikuwa mwenyekiti katika mkutano huo aliwataka viongozi wenzie kuacha porojo na kutekeleza Agizo la Raisi Kikwete kwa vitendo kuhusu kutumia fursa ya Uwanja wa Ndege wa Songwe katika kilimo cha mazao ya m,atunda, maua na mboga mboga.

 Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya TAHA, Jackline Mkindi wakati akizungumza katika Mkutano wa wadau wa kilimo cha mazao ya mboga mboga, maua na matunda kilichofanyika  katika ukumbi wa jengo la ukaguzi jijini Mbeya.
 
Wakuu wa mikoa  wakiwa makini kumsikiliza  Mkurugenzi mtendaji wa taasisiya TAHA 
 
Makatibu tawala, Wakuu wa Wilaya na wataalamu wa Kilimo wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa TAHA katika mkutano huo

Watanzania wametakiwa kubadilika kutoka kulima kilimo cha mazoea na kujikita katika uzalishaji unaolenga mahitaji ya soko la nje ili kuboresha vipato na maisha yao kutokana na uwepo wa fursa.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya TAHA, Jackline Mkindi wakati akizungumza katika Mkutano wa wadau wa kilimo cha mazao ya mboga mboga, maua na matunda kilichofanyika  katika ukumbi wa jengo la ukaguzi jijini Mbeya.

Mkindi amesema wananchi wengi hawajui kuwa kilimo hicho ni rahisi na kinaweza kubadilisha maisha yao kwa muda mfupi tofauti na mazao mengine ambayo yanachukua muda mrefu hadi kuvunwa kwake.

Amesema ni bora wakajikita katika uzalishaji wa mazao hayo wakilenga mahitaji ya soko la nje kwa kuzingatia uwepo wa fursa ya uwanja wa kimataifa wa Songwe kwa ajili ya kusafirisha mazao hayo hadi Sokoni.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro aliwataka viongozi wenzie kuacha porojo na kutekeleza Agizo la Raisi Kikwete kwa vitendo kuhusu kutumia fursa ya Uwanja wa Ndege wa Songwe katika kilimo cha mazao ya m,atunda, maua na mboga mboga.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Wakuu wa Mikoa wa Mbeya, Njombe na Iringa pamoja na makatibu tawala, Wakuu wa Wilaya na wataalamu wa Kilimo cha mazao hayo kutokana na kuwa na mpango wa pamoja katika kilimo hicho.

Na Mbeya yetu

0 comments:

Post a Comment