SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, November 10, 2013

Balozi Seif Ali Iddi katika mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa Kaskazini Mashariki ya Pacific

======================================

 Wajumbe wa Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya Kaskazini Magharibi ya Pacif Mjini Seattle wakijiorodhesha Tayari kwa kuanza mkutano wao kwenye Hoteli ya Red Lion Mjini Settle.

Mwana Habari  wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Othman Khamis akiwa katika harakati za dondoo za kutafuta mambo mbali mbali kwa ajili ya kutuma habari kwenye mkutano wa Chama cha wafanyabiashara wenye asili ya Afrika Mjini Settle Nchini Marekani alipokuwa akizungumza na mmoja wa wanajumuiya hiyo Bibi Darla Muya wa Marekani.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilakiwa kwa ngoma katika mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa Kaskazini Mashariki ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya  Red Lion kati kati ya Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini Marekani.

Burudani katika  mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa Kaskazini Mashariki ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya  Red Lion kati kati ya Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini Marekani.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubia mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa Kaskazini Mashariki ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya  Red Lion kati kati ya Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini Marekani.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiendelea kuhutubia

 Wajumbe toka Zanzibar wakibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara waliohudhuria mkutano wa 15 wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya afrika Mjini Seattle.

 Balozi Seif Iddi na wajumbe wa mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa Kaskazini Mashariki ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Red Lion kati kati ya Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini Marekani. Wa pili kulia ni Afisa Ubalozi Marekani, Bw Suleiman

Profesa Margareth Kihara Mshauri wa masuala ya wajasiri amali Mjini Seattle akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima Zanzibar Abdulla Abass wakati wa mapumziko wa Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenya asili ya Afrika Mjini Settle. Kati kati yao ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima Zanzibar  bwana Ali Aboud Mzee.

 Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar aiyevaa Kipkapa na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Ali Khalid Mirza wakibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara waliohudhuria mkutano wa 15 wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya afrika Mjini Seattle.

 Mfanyabiashara wa chama cha wafanyabiashara kutoka  Afrika Kusini Bwana Ndaba Cyril  akifurahia na kuridhika na vipeperushi vya mambo mbali mbali ya Zanzibar kwenye meza ya Wafanyabiashara wa Zanzibar katika maonyesho yaliyokuwa nje ya ukumbi wa Mikutano wa Red Lion ambao ulifanyika Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye Assili ya Afrika Mjini Seattle.

  Mwenyhekiti wa chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima Zanzibar Abdull Abass akimkabidhi zawadi maalum ya Picha inayoonyesha mandhari ya Zanzibar iliyosarifiwa kwa majani ya Gomba Mjumbe wa Baraza la Mji wa Seattle aliyemuwakilisha Meya wa Mji huo Bw. Bruce Harrel wakati wa chakula cha mchana kwenye Mkutano wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya Afrika Mjini Seattle.
 Picha zote na Hassan Issa wa OMPR.

*****
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa Bara la Afrika kuhakikisha kwamba Mataifa yaliyomo ndani ya Bara hilo yanajikita zaidi katika  mfumo mpya wa uwekezaji badala ya ile tabia ya mataifa hayo kuendelea kufanywa soko la bidhaa zinazotoka na kuzalishwa nje ya Bara hilo.

Balozi Seif alitoa kauli hiyo nzito kwenye mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa Kaskazini Mashariki ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Red Lion kati kati ya Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini Marekani.

Alisema  Bara la Afrika limebarikiwa kuwa na utajiri mkubwa wa mali asili, rasilmali pamoja na vivutio kadhaa vya utalii ambazo vikitumika vyema vinafursa ya kulipatia maendeleo makubwa na ya haraka bara hili linaloendelea kukumbwa na umaskini na maradhi.

Balozi Seif alifahamisha kwamba mkazo unapaswa kuchukuliwa na mataifa hayo katika kuona miundo mbinu ya mawasiliano, usafiri, Utalii na hata makazi yanaimarishwa ili kuongeza nguvu za uzalishaji sambamba na kuimarisha uchumi kwa ustawi wa jamii za Bara la Afrika.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliupongeza Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya Mjini Mjini Seattlle Nchini Marekani kwa mipango yake iliyojipangia ya kusaidia nguvu za uzalishaji kwa taasisi na vyama vya wafanyabiashara vya Nchi changa wakilenga zaidi Barani Afrika.

Balozi Seif aliwaomba wafanyabiashara wa Mji wa Seattle kupitia jumuiya yao kufikiria kutoa upendeleo kwa Zanzibar katika kuwekeza kwa vile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejitahidi kuimarisha miundo mbinu mbali mbali kwa lengo la kutoa fursa bora kwa wawekezaji kuwekeza maeneo tofauti ya Visiwa vya Unguja na Pemba.

Alifahamisha kwamba zipo fukwe nzuri pamoja na viungo { Spice } vinavyotoa ushawishi kwa wawekezaji wan je ya nchi kuhamasika kuwekea vitega uchumi vya katika masuala ya Utalii.

“ Sera yetu ya uwekezaji iko wazi na inatoa fursa kwa wawekezaji wote iwe  wale wa taasisi na mashirika ya kigeni na hata wale wazalendo kuwekeza katika maeneo tafauti hasa yale ya utalii ambayo Serikali yetu imeyatilia mkazo zaidi katika kudaidia uchumi wake “. Alisisitiza Balozi Seif.

Akigusia maeneo mengine kama Kilimo, Viwanda Vidogo vidogo, mazao ya viungo pamoja na Mawasiliano, Balozi Seif alisema milango iko wazi kwa wawekezaji wa Marekani kutumia fursa hiyo ili kusaidia uchumi wa Zanzibar sambamba na kuongeza ajira hasa kwa kundi kubwa la Vijana wanaomaliza masomo yao wakiwa hawana kazi za kufanya.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupitia mkutano huo aliipongeza Serikali ya Marekani kwa jitihada inazochukuwa za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar kwenye harakati zake za kujinasua kiuchumi na kujimarisha ustawi wa Wananchi wake.

Alitolea mfano wa mradi ya kataa malaria Zanzibar uliopunguza maradhi yazaidi ya asilimia 80% ndani ya Visiwa vya Zanzibar, mradi wa umeme wa wats 100, ujenzi wa bara bara zenye urefu wa kilomita 35 Kisiwani Pemba pamoja na uimarishaji wa elimu ni miongoni mwa msaada mkubwa uliotolewa na  Nchi hiyo kwa Zanzibar.

Alieleza kwamba maisha na harakati bora za kimaisha miongoni mwa wananchi wengi wa Zanzibar imefanikiwa na kukua kutokana na miundo mbinu iliyowekwa na Serikali kupitia washirika wa maendeleo yakiongozwa na lile la changamoto ya millennia la Marekani { MCC }.

Naye akitoa salamu za Chama cha wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima Zanzibar Mwenyekiti wa Chama hicho Nd. Abdulla Abass aliwaeleza wajumbe wa Mkutano huo wa Jumuiya ya wafanyabiashara wwenye asili ya Afrika kwamba  sekta ya bahari Kuu Zanzibar bado ina nafasi kubwa ya kuwekezwa na wawekezaji wa Marekani.

Nd. Abass alisema uvuvi wa Bahari kuu Zanzibar ambao unaweza kutoa ajira kubwa kwa vijana pamoja na kuongeza mapato makubwa bado haujapata uwekezaji katika kipindi kirefu.

Alisema utafiti unaonyesha wazi kwamba Bahari inayovizunguuka Viziwa vya Zanzibar bado ina utajiri mkubwa wa rasilmali inayoweza kunyanyua uchumi na mapato ya Taifa.

Mapema Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika Bwana Gishuru Peter jumuiya hiyo ilyoanzishwa karibu miaka 16 iliyopita katika mikakati yake ya baadaye imelenga kuvisaidia vyama na taasisi za wafanyabiashara zipatazo 16 barani Afrika.

Bwana Gishuru alisema hatua hiyo imepangwa ili kuziongezea nguvu jumuiya mbali mbali  Barani Afrika ziweze kujiendesha vyema kiuchumi na kustawisha jamii zinazowazunguuka.

Hata hivyo baadhi ya wataalamu waliopata fursa ya kutoa salamu na mada kwenye mkutano huo wa 15 wa jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya Kaskazini Magharibi ya Pacific Mjini Seattle walisema Bara la Afrika bado linaendelea kukumbwa na wimbi la idadi kubwa ya watu wanaozaliwa bila ya mpango.

Mtaalamu wa masuala ya takwimu kutooa chuo Kikuu cha Seattle Bwana Tonny Kelly alisema ukanda wa Mataifa yaliyomo ndani ya jangwa la Sahara umekuwa ukikabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu waliofikia asilimia 7.9% hadi mwaka huu wa 2013.

Bwana Tonny alisema kiwango hicho kikubwa kinatishia ustawi wa jamii zilizomo ndani ya ukanda huo ambacho hakiendani sambamba na  ukuaji wa uchumi wa Mataifa hayo.

Mtaalamu huyo wa masuala ya takwimu alifafanua kwamba zipo baadhi ya nchi za Afrika zinaonyesha kupata mafanikio kiasi kutokana na mpango ulioanzishwa wa   pamoja wa Kibiashara kati ya Marekani na Afrika wa { AGOA } ambao umetoa fursa kwa wafanyabiashara wa Mataifa kuuza bidhaa zao Nchini Marekani kwa mpango maalum wa mashirikiano unaozingatia unafuu wa ushuru kwa bidhaa hizo.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

9/11/2013. 

0 comments:

Post a Comment