Mratibu wa Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, Kambi Mbwana, pichani
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADAU
watano, ikiwamo Kampuni ya usafirishaji ya Phed Trans inayomilikiwa na
mdau wa muziki na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Mhandeni,
maarufu kama (Yusuphed Mhandeni), wamejitokeza kudhamini Tamasha la
Utamaduni linalotarajiwa kufanyika Handeni mjini, mkoani Tanga, Desemba
14 mwaka huu.
Wengine
waliokubali kuwezesha tamasha hilo kwa namna moja ama nyingine ni
Katomu Solar Specialist, Business Country Director (BCD) duka la mavazi
la Chichi Local War, SmartMind & Partners ambayo ipo chini ya ANESA
COMPANY LIMITED, ambapo katika tamasha hili, watadhamini kwa kupitia
kitabu cha‘NI WAKATI WAKO WA KUNG’AA’, kilichoandikwa na Albert Nyaluke
Sanga, bila kusahau kampuniutengenezaji matangazo ya Screen Masters
ambapo pia inamiliki mtandao wa Saluti5.com, ikiwa chini ya Mkurugenzi
wake Said Mdoe.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana,
alisema kuwa wadau hao ndio wa kwanza kujitokeza kuwezesha kwa tukio
hilo, huku mazungumzo yakiendelea kwa wengine wenye nia ya kudhamini
tamasha hilo.
Alisema
ishara njema imeanza kujitokeza kuwa wadau na makampuni mengi zaidi
yanaweza kuingia kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika
kwa mara ya kwanza na kuweka historia katika harakati za kukuza
utamaduni kama ishara ya kuleta maendeleo.
“Tunashukuru
kwa kampuni hizi kuwa za kwanza kuthibitisha kushiriki na sisi kwa
namna moja ama nyingine juu ya kufanyika kwa tamasha hili, hivyo naamini
kwa pamoja tutafanikisha na kuwezesha kufanya kile tunachokusudia.
“Bado
juhudi zinafanyika kuingia kwa wadhamini wengi zaidi ikiwa ni njia ya
ushirikiano kati yetu sambamba na wadau hao kuwa na nafasi kubwa ya
kutangaza biashara zao kwa Watanzania wote, hususan wakazi na wananchi
wa Handeni kwa ujumla wake,” alisema Mbwana.
Aidha,
Mbwana alitumia fursa hiyo kuwashukuru walioanza kujitokeza kudhamini
tamasha hilo na kuzitakaka kampuni, taasisi, mashirika mbalimbali pamoja
na watu binafsi wenye nia ya kukuza na kuthamini utamaduni wajitokeze
ili kuhakikisha kuwa Tamasha hilo linafanyika kwa mguso na kufikisha
kile kilichokusudiwa kwa hadhira.
Tamasha
hilo limeanza kugusa hisia za watu wengi kutokana na kuwa na mipango
thabiti ya kulifanya kwa mafanikio, ikiwa ni njia pia ya kuwakutanisha
wananchi kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kufikiria mambo ya
kimaendeleo, huku likiandaliwa na Raha Company and Entertainment.
0 comments:
Post a Comment