SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, October 9, 2013

MIKUTANO YA MWAKA YA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA NA KUNDI LA BENKI YA DUNIA YAANZA WASHINGTON DC.

 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akiwa katika majadiliano na ujumbe wa Tanzania kuhusu maandalizi ya mikutano na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa (kushoto), Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula wakimsikiliza  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile akitoa ufafanuzi.
 Waziri wa Fedha wa Zanzibar Mhe. Yusuph Mzee kulia, akisoma kwa makini taarifa zitakazowasiliswa katika mikutano hiyo wengine ni wajumbe  kutoka Tanzania.
 Toka shoto ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa, Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile, Mkurugenzi wa Idara ya kupunguza Umasikini MKUKUTA Bi. Anna Mwasha pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Harry Kitilya  wakisikiliza kwa makini.
 Ujumbe wa Tanzania wakisikiliza kwa makini hoja zinazotolewa na Waziri wa Fedha hayupo pichani ambaye ni mwenyekiti wa kikao hicho.
 Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango, Naibu Gavana wa BOT Bi. Natu Mwamba na Mchumi wa Benki Kuu Bi. Sauda Msemo  wakisikiliza kwa makini.
 Kutoka kushoto ni Kamishna wa Idara ya Sera Bw. Beda Shallanda akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dkt. Joseph Masawe.
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akimsikiliza kwa makini Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Paul Mwafongo
Ujumbe wa Tanzania katika majadiliano, kutoka kushoto ni Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Mwanaidi Mtanda, Kamishna Idara ya Sera Bw. Beda Shallanda, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dkt. Joseph Masawe na Bw. Said Magonya Kamishna wa Fedha za Nje akielezea jambo.
Picha zote na Bi. Eva Valerian – Washington DC

Imetolewa Na:
Msemaji Mkuu 
Wizar ya fedha.
Ingiahedi Mduma.

0 comments:

Post a Comment