Mkurugenzi
wa Mamlaka ya kusambaza maji Kahama na Shinyanga(KASHWASA), Ndg.Clement
Kivegaro akiwaonesha wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa
Shinyanga chanzo cha Maji kilichopo ziwani ambacho ni "Open channel"
kutoka ziwa Viktoria.kamati hiyo ilitembelea
chanzo hicho Jumatatu hii huko Ihelele wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Mhe.Rufunga
akipanda tanki la maji linalosambaza maji ya Ziwa Viktoria katika miji
ya Shinyanga na Kahama,mbele yake akiongozwa na Mkurugenzi wa KASHWASA
Ndg.Kivegaro
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama wakiendelea kuona kazi
zinazofanyika ili kuhakikisha wananchi wanaopata maji kutoka chanzo
hicho yanakuwa salama kwa matumizi.
Wajumbe
wa kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa wa Shinyanga wakisikiliza
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa KASHWASA jinsi mradi huo unavyofanya
kazi.
---
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA
Mamlaka ya kusambaza Maji katika miji ya Shinyanga na Kahama
(KASHWASA) inayoendesha mradi mkubwa wa maji ambayo chanzo chake ni Ziwa
Viktoria,ina uwezo wa kusambaza na kusafirisha maji kwa mikoa mitano
kutokana na uwezo mkubwa wa mashine za kusukuma maji pamoja na wingi wa
maji.
Hali
hiyo imebainika baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa
Shinyanga ambayo Mwenyekiti wake ni Mkuu wa Mkoa Mhe.Ally N.Rufunga,
kutembelea Ofisi kuu za mamlaka hiyo zilizopo Ihelele wilaya ya Misungwi
na Jumatatu ya wiki hii,kuona shughuli za uzalishaji na usafirishaji wa
maji kutoka kwenye chanzo cha Ziwa Viktoria.
Changamoto
kubwa iliyobainishwa na Mkurugenzi wa KASHWASA Ndg.Clement Kivegaro
wakati akisoma taarifa ya mamlaka ni uchache wa watumiaji wa maji ambapo
alisema
kwa sasa mamlaka inasambaza maji kwa asilimia 13 tu ya uwezo wake hivyo
inalazimika kuwasha pampu moja tu ya kusukuma maji, kati ya pampu tatu
zilizopo.
Kamati
iliweza
kutembelea mradi huo kwa muda wa zaidi ya saa 2 na kupata maelezo ya
kina juu ya uendeshaji na usambazaji wa maji,ambapo mradi una uwezo wa
kuzalisha maji kwa kiwango cha "cubic metres" 120,000 kwa siku.
Mradi
unauza maji kwenye mamlaka ya maji Shinyanga( SHUWASA), mamlaka ya maji
Kahama (KUWASA) na jumla kamati 45 za maji vijijini.
Mhe.Rufunga
wakati akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo amesema, lazima
serikali ihakikishe wilaya ya Kishapu nayo inapata maji ili kupanua
wigo wa watumiaji wa maji, na kuhamasisha mikoa mingine kununua maji
kutoka chanzo hicho kwa sababu pamoja na uwezo mkubwa wa mradi huo,bado
haujatumika ipasavyo kulingana na uwezo wake unaokadiriwa kulisha mikoa
zaidi ya mitano.
Amesema
pia kazi ya serikali ni kutafuta fedha ili kushughulikia matatizo
yaliyo ndani ya uwezo wa Mkoa kama kuweka mazingira mazuri kwa watumishi
wa
Mamlaka hiyo kwani chanzo hicho kipo
mbali na huduma muhimu kama hospitali, shule na maeneo ya biashara.
Na
Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga
0 comments:
Post a Comment