SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, October 7, 2013

BALOZI WA MAREKANI NCHINI AMALIZA MUDA WAKE

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na Balozi  wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Alfonso Lenhardt  na mke wake leo walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa ushirikiano aliowapa katika kipindi chao cha ubalozi hapa nchini.

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga mke wa Balozi  wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Alfonso  Lenhardt  leo walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa ushirikiano aliowapa katika kipindi chao cha ubalozi hapa nchini. Mama Salma Kikwete alikuwepo pia katika kuwaaga wanadiplomasia hao.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Balozi  wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe. Alfonso  Lenhardt  leo walipofika Ikulu kuaga na kumshukuru.
(PICHA NA IKULU)
---
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
BALOZI WA MAREKANI AMALIZA MUDA WAKE HAPA NCHINI
Tanzania na Marekani zimeimarisha mahusiano yao  katika kipindi cha miaka minne iliyopita kutokana na uhusiano na ushirikiano mzuri  wa balozi anaemaliza muda wake nchini Mh. Alfonso Lenhardt.
“Asante kwa kazi nzuri uliyoifanya katika kipindi chote cha miaka minne uliyoitumikia hapa Tanzania. Mambo mengi na makubwa yenye kuleta maendeleo na manufaa kwa Tanzania yamefanyika hapa nchini na umeyasimamia na kuyafanikisha ipasavyo”.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemueleza Balozi  Lenhardt  leo alipofika Ikulu kuaga na kumshukuru Rais na serikali yake kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi hapa nchini.
Rais Kikwete amesema ushirikiano wa nchi hizi mbili umekua na kuimarika zaidi na anatarajia kuwa balozi ajaye naye atakuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza na kuimarisha zaidi mahusiano baina ya nchi hizi.
Naye balozi Lenhart amesema Tanzania iko moyoni mwake na ataendelea kuwa balozi wa Tanzania popote alipo.
“Nikushukuru wewe mheshimiwa Rais na serikali yako kwa ushirikiano mzuri na utayari wa kunisikiliza na kunisaidia wakati wote nilipohitaji ushauri wako,  umekuwa msaada mkubwa kwangu. Asante kwa ushirikiano wako na siku zote nitaendelea kuwa balozi wa Tanzania kwani Tanzania iko moyoni mwangu”.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,

Ikulu,

Dar es Salaam.
07 October, 2013

0 comments:

Post a Comment