- . Ni muendelezo wa kampeni ya nishati ya mbadala
- .Lengo ni kusaidia wananchi kuelewa matumizi ya Umeme Jua ambao ni rafiki wa mazingira
- .Ni programu ya miaka miwili mashuleni
Na Damas Makangale, Moblog
Hoteli ya
Double Tree by Hilton ya jijini Dar es Salaam imeendelea na kampeni zake
kabambe ya matumizi ya nishati ya jua kwa kugawa taa 200 kwenye shule
ya Msingi Maskul Fundo, Jimbo la Gando kisiwani Pemba, Moblog
linaripoti.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo fupi ya kugawa taa hizo jana, Waziri wa Habari,
Utamaduni, Utalii na Michezo, Ndugu Said Ali Mbarouk ambaye ni
Mwakilishi wa Jimbo la Gando, amesema kwamba msaada huo wa Double Tree
kwa shule hiyo ni kielelezo tosha kwamba sekta binafsi zina mchango
mkubwa katika sekta ya elimu hapa nchini.
“Napenda
kuchukua fursa hii adhimu kuwashukuru uongozi na wafanyakazi wote wa
Double Tree kwa msaada wao mkubwa kwa shule yetu ya hapa Gando ambapo
watoto wetu watasoma katika mazingira rafiki yatayowawezesha kufaulu
mitihani yao,’ alisema Mbarouk.
Waziri
Mbarouk amesema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Serikali,
wananchi na wadau wote wa maendeleo hawawezi kuendelea kutegemea umeme
wa vyanzo vya maji na badala yake umeme wa jua ambao ni nishati mbadala
ni ufumbuzi wa tatizo la nishati nchini.
Amesema
mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi hasa kwenye nishati ni
muhimu kwa sababu ni nishati ndio injini ya Uchumi wa taifa lolote lile
hapa duniani kwa sasa.
‘lakini
kampeni hizi zitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi kutambua na kuelewa
nishati mbadala na umuhimu wake katika maisha ya kila siku ikiwemo
mazingira,” alisisitiza
Hoteli ya
DoubleTree ilizindua rasmi kampeni ya matumizi ya nishati ya jua ambayo
itadumu kwa muda wa miaka miwili katika shule za msingi nchi nzima miezi
kadhaa iliyopita.
DoubleTree
itakuwa ikigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa
wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa
nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme
ambacho ni rafiki wa mazingira kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao.




0 comments:
Post a Comment