SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 24, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA UTOKOMEZAJI WA UGONJWA WA FISTULA, JIJINI DAR

 Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwasili katika eneo lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kufanyia shughuli za maadhimisho hayo.  Makamu wa Rais Dkt Bilal, akimjulia hali mtoto mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baba wa mtoto, Elizabeth Nora kutoka Dodoma aliyelazwa katika Hospitali ya CCBRT, wakati Makamu alipofika hospitalini hapo jana Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika  Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dokta wa Hospitali ya CCBRT, wakati alipokuwa akitembelea katika wodi za wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo, alipofika hospitalini hapo jana Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula. Kulia ni Mtoto Boniface Patrick akiwa na Baba yake, Patrick Luwao, Wakazi wa Dodoma, akiwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji na kuongezewa sehemu ya mguu uliokuwa mfupi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Stellah Nzyemba, ambaye awali alikuwa mgonjwa na baada ya kutibiwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT na kupona ameajiriwa ili kuwasaidia wagonjwa wa Fistula. Makamu alifika hospitalini hapo  jana Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.    Balozi wa Ugonjwa wa Fistula, Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Mwana FA, akisoma hotuba yake kuhusiana na kuzunguka katika baadhi ya mikoa na kutoa ujumbe kwa wananchi na hasa kina mama kuhusu Ugonjwa huo.  Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose, akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula, yaliyofanyika jana Mei 23, 2013 Jijini Dar es Salaam.
Wasanii 21 walioungana na kuimba wimbo wa Kidole kimoja,wakitoa burudani jukwaa .
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

0 comments:

Post a Comment