Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China Zanzibar Bibi Chen Qiiman akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif Ali Iddi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyopo ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China inatarajia kuikabidhi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jengo jipya la Skuli ya Msingi ya Mwana kwerekwe C katika kipindi cha siku chache zijazo baada ya kukamilika ujenzi wake.
Ujenzi huo umekuja kufuatia ziara ya aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu wa China Bw. Hui Liangyu ambae ameshastaafu aliyoifanya Zanzibar na kutia saini Mkataba kati ya serikali yake na Zanzibar katika masuala ya Uchumi na Ufundi ukiwemo pia mradi huo wa ujenzi wa skuli ya Mwanakwerekwe C.
Mkataba huo uliotiwa saini umelenga kuipatia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jumla ya RMB Milioni Sitini { 60,000,000 } sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 14.8 ambapo kati ya fedha hizo ujenzi wa skuli hiyo pekee umegharimu jumla ya dola za kimarekani Milioni 1.6.
Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Bibi Chen Qiiman alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif Ali Iddi hapo Katika Ofisi yake iliyopo katika Jengo la Baraza la Wawakilishi liliopo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment