SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, March 27, 2013

CHADEMA yasaini Mkataba wa Ushirikiano na Conservatives ya Denmark



Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesaini mkataba wa ushirikiano na Chama cha Conservative cha watu wa Dermark. MKataba huo una lengo la kuwajengea uwezo Vijana na Wanawake zaidi ya 30,000 kwa njia ya mafunzo mbalimbali kupitia mabaraza yao ya Vijana na Wanawake. Mkataba huo utagharimu takribani kiasi cha Tsh Milioni 400


Akisaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa amesema wamefanya shughuli hiyo mbele ya waandishi wa habari na kuweka hadharani mkataba huo ili kuonyesha uongozi wa mfano kwani CHADEMA imekuwa ikiitaka mikataba yote inayosainiwa kwa niaba ya wananchi kuwekwa hadharani ili wananchi waweze kuitambua na kuielewa. 

 Dk. Slaa ameongeza kuwa wanafanya mambo yao kwa uwazi ili kuepuka propaganda zinazofanywa na serikali kupitia usalama wa taifa pamoja na Chama Cha Mapinduzi juu ya ushirikiano ambao CHADEMA imekuwa ikiupata kutoka kwa vyama rafiki duniani. CHADEMA ni mwanachama wa umoja wa vyama vya kidemokrasia duniani unaojulikana kama IDU. 

Walioshuhudia utiani saini huo ni Makatibu wakuu wa Baraza la Vijana, Deogratius Munishi na wa Baraza la Wanawake, Naomi Kaihula. Wengine ni wakurugenzi na maofisa mbalimbali wa CHADEMA makao makuu.
 Picha na Kurugenzi ya Habari Chadema.
CHANZO GPL

0 comments:

Post a Comment