SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, March 28, 2013

Bei ya vyakula Dar yashika kasi kipindi cha Pasaka

Na Goodluck Eliona na Pamela Chilongola
Bidhaa zilizopanda kwenye masoko mbalimbali jijini Dar es Salaam ni mchele, nyanya, viazi karoti na unga wa sembe.

Dar es Salaam. Wakati Wakristo nchini wakijiandaa kuungana na wenzao duniani kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, bei ya  vyakula jijini imezidi kupanda kutokana na  sababu mbalimbali.

Akizungumza sababu ya kupanda kwa bei hizo mfanyabiashara wa Soko la Kisutu, Japheti Kibiriti alisema moja ya sababu ni baadhi ya magari yanayosafirisha bidhaa kukwama njiani kitokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Alisema bidhaa zilizopanda kwenye masoko mbalimbali jijini Dar es Salaam ni mchele, nyanya, viazi karoti na unga wa sembe.

Kibiriti alisema bei ya nyanya imepanda ambapo tenga la ndoo mbili za plastiki  sasa linauzwa kwa Sh50,000 kutoka Sh30,000.

Mchele unauzwa Sh2,400 hadi Sh2,600, karoti Sh2,000, viazi vinauzwa kwa Sh2,000, unga wa sembe kilo moja huuzwa Sh1700 huku pilipili hoho zikiuzwa kwa kilo moja  Sh3,000.

Mfanyabiashara wa  Soko la Buguruni, Bakari Mponda alisema mkungu mmoja wa ndizi huuzwa kuanzia Sh22,000 hadi  Sh30,000 awali mkungu huo ulikuwa unauzwa kwa Sh15,000.

Mponda alisema bidhaa zingine zilizopanda ni matunda mbalimbali na hiyo inasababishwa na magari kukwama njiani hivyo bidhaa nyingi kuharibika.
Kwa upande wa nguo, Debora Sanze ambaye alikuwa akinunua nguo za watoto katika eneo la  Kariakoo alisema bei aliyoikuta haikuwa mbaya sana.

“Sioni tofauti ya bei na nilivyozoea kununua sikukuu zilizopita, labda kwa sababu nimezoea kununua duka moja,” alisema Sanze.
CHANZO: BOFYA

0 comments:

Post a Comment