SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, March 3, 2012

AIRTEL NA USALAMA BARABARANI


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Kagasheki (wa tatu kutoka kulia
mwenye miwani) akishirikiana na viongozi wa Usalama barabarani pamoja
na viongozi wa Club ya Rotary ya Dar es Salaam kubandika machapisho ya
Usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Airtel
kushirikiana na Club ya Rotary yenye ujumbe wa kuhakikisha kuwa
madereva wanaendesha kwa usalama zaidi bila kutumia siku za mkononi.
Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani
Mh. Mohamed Mpinga, muwakilishi kutoka Club ya Rotary Dar es Salaam,
Bw. Zainul Dossa pamoja na Bw. Hamza kassongo.


Serikali imesema kutokuwepo kwa sheria ya barabarani inayozuia
matumizi ya simu za mkononi wakati wa uendeshaji wa vyombo vya moto
kunachangia kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria madereva ambao
waonekana kutumia simu za mkononi huku wakiwa wanaendesha vyombo
hivyo.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa mambo ya ndani Balozi Hamis
kagasheki wakati wa zoezi la kubandika ujumbe katika magari mbalimbali
unaokataza matumizi ya simu za mkononi wakati wa kuendesha vyombo vya
moto.
Ni kweli hadi sasa hakuna sheria inayomkataza moja kwa moja dereva
kuacha kutumia simu awapo barabarani lakini naomba wananchi wafahamu
kuwa hili linafanyiwa kazi na wafuate maelekezo yalioyotolewa na wadau
kama hawa ambayo kiukweli yanatoa elimu ya kupunguza madhara ya ajali
za mara kwa mara” alisema Balozi Khagasheki
kwa mujibu wa tathmini ya jeshi la polisi baadhi ya ajali nyingi
zinazotokea barabarani zinatokana na matumizi ya smu za mkononi wakati
wa kuendesha vyombo vya moto hali inayopelekea kuongezeka kwa ajali
nyingi na kusababisha vifo ambavo vingeweza kuzuilika kwa urahisi.
Balozi kagasheki amesema kuwa upungufu wa kutokuwa na sheria ya kuzuia
matumizi ya simu za mkononi wakati kuendesha gari unapelekea
kushindwa kuwachukulia hatua kali madereva ambao wanaonekana kufanya
hivyo.
Naye muandaaji wa zoezi hilo Zeinul Dossa kutoka klabu ya Rotary ya
jijini dare s salaam pamoja na Jene matinde afisa uhusiano wa kampuni
ya smu za mkononi ya Airtel wamesema kuwa zoezi hilo la kubandika
ujumbe huo litafikisha ujumbe kwa madereva wengi pamoja na kupunguza
ajali.
Zaidi ya machapisho elfu 5 yametengenezwa kwa ajali ya kubandika
pamoja na kusambazwa katika magari mbalimbali ambayo yatarahisisha
kupunguza ajali za barabarani ambazo zinaweza kuzuilika kwa
kshirikiana na jeshi la polisi.

0 comments:

Post a Comment