SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, October 26, 2011

MRADI WA VODACOM"MWEI"JINSI UNAVYOWAINUA WAKINAMAMA NCHINI TANZANIA

Meneja wa Mradi wa  MWEI unaoendeshwa na Vodacom Tanzania Mwamvua Mlangwa,akiongea na wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa  kijij cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,kabla ya kuanza kuwapatia  mikopo ya fedha taslimu zinazotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake  wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini na kurudisha fedha hizo bila riba.
 Meneja wa Mradi wa  MWEI unaoendeshwa na  Vodacom Tanzania Mwamvua Mlangwa,akimpatia Mwanaidi  Musa  mkopo wa fedha taslimu       kwa ajili ya kufanyia biashara zake na kuzirudisha fedha hizo bila riba yoyote,aliyekaa kushoto ni Mratibu wa Mfuko huo Ally Mbuyu.
Wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa  kijij cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,wakimsikiliza Meneja wa Vodacom Tanzania  wa  Mradi wa  MWEI Mwamvua Mlangwa hayupo pichani ,wakati  wakisubiri kupatiwa mikopo yao ya  fedha taslimu zinazotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini bila riba.
Wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa  kijiji cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,wakiwa wameketi wakisubiri kupatiwa mkopo wa fedha taslimu unaotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini bila riba. 
Na H@ki Ngowi.

0 comments:

Post a Comment