SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, June 24, 2011

ZIFF KUMUONA SHAGGY LAKI MOJA NA KIWANGO CHA CHINI 15,000!!

Shaggy.
Na Andrew Chale, Zanzibar.
 KUTUA NA BOTI MAALUM VISIWANI ZANZIBAR.
Mwanamuziki wa kimataifa wa ragga na mshindi wa tuzo za Grammy 2011, Orville Richard   ‘Shaggy’  usiku wa leo anatarajia kupanda jukwaani ndani ya Ngome kongwe ukumbi wa Mambo kutumbuiza shoo kali huku akisindizwa na wanamuziki nyota wa hapa nchini sambamba na kundi la THT Dancers.
Kwa mujibu wa  Meneja masoko  na mmoja wa waratibu wa Tamasha la Filamu za Nchi za majahazi maarufu  ZIFF,  Laurian Kipeja  alisema kuwa, mwanamuziki huyo wa kimataifa atapanda jukwaani  hiyo  majira ya usiku na kupiga shoo kali na  ya aina yake huku akisindikizwa na wasanii mahiri wa hapa nchini.
Kipeja alisema kuwa, tayari tiketi za shoo hiyo zimeanza kutolewa katika  ofisi zilizopo makao makuu ya ZIFF ndani ya Ngome Kongwe huku bei zikiwa nafuu kwa kila mmoja.
“Shoo hii itakuwa ni ya pekee na ya aina yake kwa wakazi wa Zanzibar na wageni mbalimbali huku kima cha juu kwa V.I.P. wa juu ni  laki moja (100000) na V.I.P wa kawaida   (50,000)  na vya kawaida kwa wageni ni 30,000 huku  wazawa ama wakazi ni 15,000” alisema Laurian.
Aidha, inadaiwa Shaggy  atatua visiwani hapa na boti maalum mapema leo na kisha saa sita mchana atafanya mkutano na vyombo vya habari  sambamba na kufunga vyombo kwenye hoteli ya Zanzibar Resort.
Kwa upande wake,meneja wa ZIFF, Danny Nyalusi alisema wasanii watakao msindikiza Shaggy ni pamoja na Sultan King, na kundi la THT ambapo watapiga shoo kali ambayo haijawai kutokea visiwani humo.
Pia alisema kuwa kwa mwaka huu, kaulimbiu ya ZIFF imebeba ujumbe wa ‘A SEASON OF VISIONS’  na kwa mara ya kwanza, tamasha hilo limedhaminiwa na  mdhamini mkuu Kampuni ya Bia ya Serengeti, kupitia kinywaji chake cha Tusker Malt, Prime Time promotion, Coconut FM, Azam Marine Co ltd, TTB, Common Wealth Foundation, Coca-Cola, GIZ (TZ), na Ujerumani, Smole, Movenpick, Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa.

0 comments:

Post a Comment