SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, June 24, 2011

TANZANIA YAPATA TUZO YA UN KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA JAMII!!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu Stephen Wassira  Tuzo  ya UN  ya mshindi wa pili ya Tanzania katika kutoa huduma bora kwa Jamii (Mkurabita) wakati Makamu alipofika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Juni 23, 2011 kufunga maadhimisho ya siku ya Utumishi ya Umoja wa Mataifa na Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hafla hiyo kuadhimishwa Barani Afrika na kufanyika nchini Tanzania.
Walipata tuzo hawa ni kutoka Ubalozi wa Afrika ya Kusini, wakifurahia tuzo yao kwa pamoja baada ya kukabidhiwa.
Balozi wa canada nchini, akipokea tuzo kwa niaba ya nchi yake.
Zoezi la kukabidhi tuzo linaendelea kwa wawakilishi wa nchi mbalimbali.
Wafanyakazi wa Ubalozi wa Afrika ya Kusini nchini, wakifurahia tuzo yao baada ya kukabidhiwa.
Baadhi ya watu kutoka mataifa mbalimbali walioshiriki wakati wa hafla hiyo ya kutoa tuzo na kufunga maadhimisho hayo katika Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
(Picha na Muhidin Sufiani-OMR).

0 comments:

Post a Comment