Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam akifungua warsha kuhusu Mahitaji na Vikwazo katika
Upatikanaji wa Huduma za Kifedha Tanzania iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam katika kituo cha Utafiti cha ESRF, ambapo amewataka wasomi na
wataalam nchini kutumia matokeo ya tafiti mbalimbali kuisadia Serikali
katika kutimiza malengo ya kimaendeleo haswa katika kuboresha sekta ya
huduma za kifedha. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha ESRF Bohela
Lunogelo na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa Theresia Mmbando.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha ESRF Bohela Lunogelo akimkaribisha mgeni rasmi
kufungua warsha hiyo ambapo amefafanua lengo kuu la utafiti huo kuwa ni
kutoa msaada wa serikali, watunga sera, watoa huduma za kifedha kwenye
mabenki, taasisi binafsi, watafiti, wasomi na jumuiya ya wafadhili kwa
ujumla. Katikati ni mgeni rasmi Jordan Rugimbana na Kushoto ni Katibu
Tawala Mkoa Theresia Mmbando.
Wadau kutoka Taasisi mbalimbali wakifuatilia presentation iliyokuwa ikionyesha matokeo ya utafiti huo.
Mmoja
wa watafiti Vivian Kazi (kushoto) akiwasilisha presentation ya kwanza
ya utafiti wa FinScope 2009 juu ya mahitaji na vikwazo katika
upatikanaji wa huduma za kifedha nchini. Huu ni utafiti wa pili wa aina
hii kufanyika Tanzania ambapo wa kwanza ulifanyika mwaka 2006. Katikati
ni Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi wa ESRF Dkt. Donatila Kaino.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti juu ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii
Tanzania (ESRF) Bohela Lunogelo (wa kwanza kulia waliokaa) katika picha
ya pamoja na washiriki wa warsha ya Mahitaji na Vikwazo katika
Upatikanaji wa Huduma za Kifedha nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment