SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, June 6, 2011

BINTI AHITAJI MSAADA WA WASAMARIA WEMA KUMNUSURU!!

Mtoto Cecilia Edward.
Mtoto Cecilia Edward mkazi wa Mbagala Kuu – Njiang’ombe anayesumbuliwa na maradhi ya moyo yanayosababisha tumbo lake kuwa kubwa, kupitia kwa mlezi wake ameomba wasamaria wema wajitokeze kumsaidia kuweza kupata matibabu na mahitaji mengine muhimu.
Mtoto huyo anayetakiwa kwenda kutibiwa India, aliyekuwa akiishi Kisarawe katika kijiji cha Mpigi, alizaliwa na matatizo hayo mwaka 1995,baada ya kufiwa na baba yake aliyekuwa akiitwa Edward, majukumu yote ya kumhudumia yalibaki mikononi mwa mama yake Helena Mbago.
Matatizo ya mtoto huyo yalijitokeza zaidi mwaka 2000 baada ya mama yake mzazi aliyekuwa akimtunza nae kufariki baada ya kuugua, hali iliyopelekea kukosekana huduma muhimu ikiwemo kushindwa kuendelea na masomo.
Mtoto Cecilia mwenye umri wa miaka ‘14’ kwa sasa anaishi na msamaria mwema Kambaliko Nyarungembe mkazi wa Mbagala Kuu – Njiang’ombe.
Aidha mtoto huyo pamoja na mlezi wake wameelezea kusikitishwa kwao na kitendo cha mtoto Cecilia kuzushiwa habari na gazeti la UWAZI –Toleo la 687 la tarehe 31 Mei – Juni 6, 2011 ambapo hawakufurahishwa na namna habari ya mtoto huyo ilivyoandikwa ikiwa ni pampoja na kutumia picha yake.
Pia wamelitaka gazeti hilo kumuomba radhi mtoto huyo kupitia ukurasa ule ule walioandikia habari hiyo.
Kwa wasamaria wema watakaokuwa tayari kusaidia binti huyu kwa ajili ya kumuwesha kupelekwa India kwa matibabu na pia kuweza kupata mahitaji muhimu ya kila siku kama vile chakula, nguo na mengine ikiwemo kumlipia hospitali kwenda kunyonywa maji tumboni wawasiliane na mlezi wake Bw. Kambaliko Nyarugembe kupitia simu namba 0715 – 095797 na 0762 – 962467.

0 comments:

Post a Comment