SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 21, 2011

Rais Jakaya Kikwete Ashiriki Mazishi Ya Sheikh Yahya Hussein!!

Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Sheikh Yahya Hussein aliyezikwa katika Makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akibadilishana mawazo na viongozi wa dini kabla ya kuwasili kwa mwili wa aliyekuwa Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein katika makaburi ya Tambaza jijini Dar. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadiki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akisikiliza mawaidha wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein aliyefariki dunia jana jijini. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki. 
Mwili Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein ukisubiri kushushwa kaburini tayari kwa maziko. 
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mtoto wa mwisho wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein aliyezikwa leo katika makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam. 
 Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki kumzika Mnajimu Mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati.
Mziwanda wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein akitia udongo kwenye kaburi la baba yake wakati wa mazishi. 
Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Suleiman Kova akishiriki Mazishi ya Sheikh Yahya Hussein aliyezikwa leo Alasiri jijini Dar. 
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia uratibu na uhusiano Mh. Steven Wassira akishiriki katika mazishi ya Mnajimu Mashuhuri wa Afrika ya Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein. 
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM taifa Mh. Nape Mnauye akishiriki katika mazishi ya Sheikh Yahya Hussein. 
 Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akiwasili nyumbani kwa Marehemu Sheikh Yahya Hussein.
Mamia ya waombelezaji wakisiliza mawaidha nyumbani kwa marehemu Sheikh Yahya Hussein. 
Wakinamama wakionekana na huzuni kubwa ya kuondoka kwa kipenzi cha wengi Sheikh Yahya Hussein. 
 Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akitoa wasifu wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein.
 Mwenyekiti wa Chama cha CUF Prof. Ibrahim Lipumba akitoa wasifu wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein.
 Mwili wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein ukiswaliwa nyumbani kwake kabla ya kuelekea makaburini.
Kinamama wakilia kwa uchungu msibani.
Msafara wa kuelekea makaburini ukiongozwa na mapikipiki.
Umati wa waombelezaji ukielekea makaburini.
(Picha na Geofrey Mwakibete-Mo Blog)

0 comments:

Post a Comment