SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 25, 2011

Mkutano Wa Siku Tatu Wa Uwazi Na Uwajibikaji Katika Bajeti Kwa
Nchi Za Afrika Mashariki 
 Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Ludovick Utouh akizungumza na waandishi wa Habari  (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa ukaguzi wa mahesabu katika mashirika ya umma na umuhimu wa uawajibikazi kwa wananchi na ushirikishwaji wa taasisi mbali mbali katika kuandaa bajeti. Utouh alisema kuwa anaridhishwa na jinsi serikali inavyoshughulikia mapendekezo yake juu ya masuala mbali mbali yanayohusiana na uthibiti na ukaguzi wa hesabu.
Waziri wa Afrika Mashariki Samweli Sitta akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  katika ukumbi wa Ubungo Plazza kuhusu umuhimu wa Serikali za Afrika Mahariki kuwa wazi kwa wanachi kuhusu bajeti zake na mipango endelevu ya bajeti hizo katika kupigana na umaskini wa kipato.Sita alisema kuwa Tanzania ni nchi inayofanya vizuri miongoni mwa nchi za Afrika Mshariki katika uwazi na uwajibikaji wa mahesabu ya Serikali kwa wananchi wake.
 Mbunge wa Bariadi  Magharibi Andrew Chenge akiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Fedha na uchumi Abdal Kigoda akitoa mada juu umuhimu wa uwazi na uwajibika katika  bajeti za serikali.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Uwazi na uwajibikaji wa mahesabu ya Serikali za nchi za Afrika Mashariki. Mkutano huo  ni wa siku tatu, unatarajiwa kufungwa mei 25 na umewajumuisha wawakilishi kutoka tasisi mabali mbali wakiwemo  Wabunge, Wenyeviti na wajumbe wa kamati za Fedha za Bunge,  wawakilishi kutoka Benki ya Dunia, wadau wa mashirika ya Maendeleo, Wahisani na Waandishi wa habari.
Mgeni rasmi katika mkutano wa siku 3 wa kujadili uwazi na uwajibikaji katika bajeti kwa nchi za Afrika Mashariki ambae pia ni Waziri wa Afrika Mashariki Samweli  Sitta wa tatu kulia akijadili jambo na Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Ludovick Utouh. Wengine ni Mwenyeketi wa kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi Abdalah Kigoda  wa kwanza kulia, Mbunge wa Bariadi na mwenyeketi wa kamati ya Bunge ya Hesabu Za  Serikali John Cheyo wa pili kulia wakiwa katika mkutano wa  siku tatu wa kujadili uwazi na uwajibikaji katika bajeti za nchi za Afrika Mashariki juzi asubuhi katika ukumbi wa Ubungo Plazza. 

0 comments:

Post a Comment