SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 20, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA WAUGUZI MNAZI MMOJA DAR!!


 Makamu wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisoma hotuba yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salam leo Mei 20. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimkabidhi zawadi, Paul King’ara Muuguzi kutoka mkoani Mwanza wakati wa maadhimisho ya Sherehe za ya miaka 40 ya kuzaliwa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salam leo Mei 20. 
 Catherine Magole, akikabidhiwa zawadi. 
 Wauguzi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salam leo Mei 20. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Muuguzi mstaafu Jito Ramu, aliyekuwa mmoja kati ya wauguzi waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salam leo Mei 20. Dkt Bilal alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo. 
 Wimbo wa Taifa 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wenyeviti wa Mkoa na Wauguzi wakuu wa Hospitali za Mikoa.  
 Wauguzi waliohudhuria sherehe hizo wakila kiapo mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa sherehe hizo. 
Baadhi ya wauguzi wakiserebuka kushangilia sherehehe hiyo wakati msanii wa muziki Mrisho Mpto, walipokuwa akitoa burudani kwenye sherehe hizo. 
( Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu wa Rais).

0 comments:

Post a Comment