SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 23, 2011

TAIFA STARS KUKIPIGA NA MSUMBIJI LEO MAPUTO

Taifa Stars
Stars iliwasili jana salama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo saa 5.52 asubuhi (saa 6.52 kwa saa za nyumbani) kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Nairobi. Timu iko hapa kwa ajili ya mechi ya ufunguzi wa Uwanja wa Taifa. Uwanja huo mpya ambao capacity yake ni watazamaji 40,000 umejengwa na Wachina na uko nje kidogo ya Jiji la Maputo ambapo ni wastani wa saa moja kwa gari kutoka mjini. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa uwanja huo ambao ndiyo utakaotumika kwa michezo ya All Africa Games Septemba mwaka huu atakuwa Rais wa Msumbiji wakati Rais Jakaya Kikwete anawakilishwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi. Timu imefikia hoteli ya VIP Grand ambapo jana saa 12.30 kwa saa za hapa ilifanya mazoezi Uwanja wa Taifa kwa dakika 45. Mechi itaanza saa 12.30 jioni kwa saa za hapa, na itachezeshwa na waamuzi kutoka Swaziland. Mwamuzi ni Simanga Hhleko wakati wasaidizi wake ni Bhekisizwe Mkhabela na Lybnah Sibiya. Fourth official ambaye ni wa hapa Msumbiji ni Estevao
Matsinhe.
Taifa Stars line up;
Shabani Dihile (1)
Shadrack Nsajigwa (14)- captain
Amir Maftah (3)
Aggrey Morris (6)
Nadir Haroub (13)
Nurdin Bakari (5)
Mohamed Banka (16)
Shabani Nditi (19)
John Boko (9)
Machaku Salum (11)
Mwinyi Kazimoto (22)

Substitutes:
Shabani Kado (18)
Kigi Makasi (7)
Julius Mrope (8)
Ramadhan Chombo (21)
Jabir Aziz (12)
Mbwana Samata (10)
Juma Nyoso (4)
Officials: Jan Poulsen- Head Coach Sylvester Marsh- Assistant Coach Juma Pondamali- Goal keeping Coach Leopold Tasso- Team Manager Dr Mwanandi Mwankemwa- Team Physician Alfred Chimela- Kit Manager Timu itaondoka hapa kurejea nyumbani kesho April 24 saa 11.35 kwa Kenya Airways hadi Nairobi ambapo itakaa kwa muda ikisubiri kubadili ndege kwa ajili ya safari ya Dar es Salaam. My contact in Maputo +258 767 310242 Boniface Wambura Media Officer Tanzania Football Federation

0 comments:

Post a Comment