SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 23, 2011

HABARI KAMILI YA KUUWAWA KWA KATIBU WA CCM IRINGA

Damu zikiwa zimetapakaa eneo la mauwaji.
Mjane wa marehemu.
Wananchi wakiwa nyumba kwa marehemu.
Marehemu enzi za uhai wake
WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamemuua kwa mapanga katibu mwenezi wa CCM kata ya Mgama wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa Patrick Ng’ara (40).

Katibu wa CCM wilaya ya Iringa vijijini Mohamed Dhikri alisema kuwa mauwaji hayo yamefanyika usiku wa kuamkia ijumaa kuu na kuwa katibu huyo na kuwa chama chake kimepoteza kiongozi mchapa kazi.

Alisema kuwa kifo cha katibu huyo kimekuja huku kukiwwa na mvutano mkubwa kati ya viongozi hao na wale wa wilaya ,mkoa na Taifa baada ya diwani wa kata hiyo Lupala kumvaa naibu katibu mkuu Chiligati kuwa kati ya watu ambao walitegemewa kuvuliwa magamba ndani ya CCM naibu katibu mkuu huyo ni moja wapo na kuwa hakutegemea kumwona akiwa kiongozi ndani ya CCM.

Mjane wa marehemu huyo Tumain Ndendia (36) alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 2.45 usiku wakati katibu huyo akitoka katiika vikao vya chama .

Alisema kuwa wakati tukio hilo likitokea yeye na mtoto walikuwa ndani akijiandaa kulala na ghafla alisikia sauti ya kishindo nje mfano wa kitu kuanguka chini na baada ya kutaka kutoka alisikia sauti za watu hao zaidi ya wakishauriana kuingia ndani kufanya mauwaji kwake .

Hata hivyo alisema pamoja na kumuua katibu huyo bado hawakuweza kuchukua kitu chochote na hata piki piki ambayo alikuwa nayo waliiacha eneo la tukio ikiwa haijazimika.

Katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Pius Pukapuka alisema kuwa juzi jioni yeye alifika katika kijiji cha Ilandutwa na kumkuta katibu huyo kwa ajili ya kumfikishia barua ya kikao cha chama kinachotaraji kufanyika kesho na kumkuta akiwa katika kikao cha chama ngazi ya kata akiongoza .

Mbunge wa jimbo la kalenga Dr .Wiliam Mgimwa alisema kuwa katibu huyo alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wazuri ndani ya CCM na kuwa kifo chake ni pengo kubwa ndani ya chama na kuwa bado suala hilo wanaliachia mikononi mwa polisi.

Hata hivyo diwani wa CCM kata ya Mgama Denis Lupala alisema kuwa kwa upande wake katibu huyo alipata kuwa naye katika kikao wakitathmini ziara ya Naibu katibu mkuu wa CCM Taifa John Chiligati katika kata hiyo ya Mgama.

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limethibitisha kutokea kwa mauwaji hayo kupitia kwa kamanda wa polisi wa mkoa Evarist Mangalla na kuwa msako mkali unaendeshwa dhidi ya wauwaji hao
**************************
DIWANI WA CCM ALIYEMWITA CHILIGATI FISADI KUHUKUMIWA LEO
Diwani wa kata ya Mgama wilaya ya Iringa vijijini Bw.Denis Lupala (pichani)ambaye juzi alimwita Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara John Chiligati kuwa ni fisadi na alipaswa kuvuliwa gamba mjini Dodoma amepewa barua ya kuitwa katika sekretarieti ya wilaya /usalama na maadili ili kujadiliwa kwa utovu wa nidhamu ,diwani huyo anatakiwa kufika leo majira ya saa 4 asubuhi katika ofisi za CCM huku mwenyewe akijigamba kuwa yupo tayari kuondoka ndani ya CCM iwapo atazibwa mdomo kwa kusema ukweli.
Na Francis Godwin.

0 comments:

Post a Comment