SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, April 7, 2011

SERENGETI FIESTA SOCCER BONANZA 2011 MWANZO MZURI

Michezo hiyo iliweza kuanza kwa maandamano kuanzia viwanja vya BIAFRA kinondoni mpala leaders kama unavyoona katika picha
Leo Mashabiki wa Tanzania wa timu maarufu duniani baadhi yake zikiwa Arsenal, Manchester United, Liverpool na Chelsea za Uingereza, na Inter Milan ya Italia, walichuana katika mtanange uliotoa burudani ya kutosha katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam Serengeti Fiesta soccer bonanza 2011.
Ikiwa ni awamu ya kwanza kabisa ya Serengeti Fiesta soccer bonanza ambapo timu mbali mbali zimepata kushindanishwa.
Burudani hiyo ambayo ilivutia umati mkubwa wa mashabiki ilipokelewa kwa furaha kubwa hususani katika sikukuu ya Siku ya Karume ambayo ni leo.
mashabiki watimu mbali mbali walijiunga nasi kuandamana kuelekea viwanjani.Ushabiki hapa mwanzo mwisho.
Hakuna kuogopa mvua vijana wanagangamala.
Timu zilizoshindanishwa na bado zinaendelea kushindanishwa na kuibuka na ushindi ni
  • CHELSEA 2 LIVERPOLL 0
  • INTERMILAN 0 BARCELONA 1
  • MAN UNITED 1 REALMADRID 3
  • AC MILAN 3 BARCELONA 2
  • ARSENAL 0 NA AC MILAN 1
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhuu8GFwKxFxUHcgcEqoLcJpiqJORcKbBrkc18KfLKKekIUu6xBmeWHOBYvYDWXmUrez34hbI23edMfoYpUX4QRMy73ieB8jTipwd4DDD8L3X51k2mxOv-oAHtW5ktssC7-9YSfMgSae48n/s1600/6.jpg
Mratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta soka bonanza,Shafii Dauda akitangaza mshindi kwenye michuano ya mashabiki wa vilabu huko ughaibuni,iliofanyika jioni ya leo kwenye viwanja vya Readers Club na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Katika michuano hiyo iliyohusisha timu nane(8).
Real Madrid ndiyo iliyonyakua ushindi kwa kuibuka na kitita cha sh Mil Moja pamoja na kombe,ikifuatiwa na timu ya Chelsea kwa kuibuka na kitita cha sh Lakini 5.

0 comments:

Post a Comment