SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, November 10, 2010

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais wa Guinea yaonyesha kuwepo mchuano mkali!!
Baada ya kuhesabiwa asilimia kumi ya kura za duru ya pili ya uchaguzi mkuu wa rais wa Guinea uliofanyika siku ya Jumapili matokeo yanaonyesha kuwa kura za wagombea wawili wa kiti hicho zinakaribiana. Tume ya uchaguzi ya Guinea imetangaza kuwa matokeo hayo yanayojumuisha majimbo matano tu kati ya 38 ya nchi nzima pamoja balozi 12 za nchi hiyo nje ya nchi yanaonyesha kuwa Waziri Mkuu wa zamani Cellou Dalein Diallo anaongoza kwa kujipatia kura 167, 725 dhidi ya Alpha Conde ambaye amepata kura 156,877. Tume ya uchaguzi ya Guinea imesema imeamua kutangaza matokeo hayo kila siku mara baada ya kuyapokea kutoka vituoni.

0 comments:

Post a Comment