Kutoka Udosini:Jumba la Kwanza la Dola Bilioni Duniani
Mukesh
Ambani, ni tajiri bilionea kuliko wote nchini India, na pia ni tajiri
wa nne kwa thamani katika levo za dunia. Ambani amejijengea jumba la
kuishi lenye thamani za Dola Bilioni za Kimarekani.
umba hili lina ghorofa 27 ambazo ukizizungukia zote kwa siku moja basi unamaliza mahitaji yako karibu yote bila kutoka nje ya mjengo huo. Mukesh amesema kwamba hili ni jumba la kuishi yeye, mkewe kipenzi, na watoto wao watatu (Hapa lazima mwafrika apige kelele).
Katika jumba hili kuna sehemu maalum kwa ajili ya kufanyia mazoezi na kutunza afya kwa ujumla, mahala pa kuchezea dansi penye ukubwa kama wa klabu zetu tunazozifahamu hapa nyumbani, madimbwi kadhaa ya kuogelea (swimming pool), ukumbi wa kutazamia senema unaoweza kubeba watu 50 kwa wakati mmoja, vyumba kibao vya wageni (mwafrika sijui ataendelea kulalama kwenye hili?), na mwisho kabisa ni varanda zenye ukubwa wa kucheza sarakasi kabisa.
Ukitaka kufika nyumbani kwa bwana Mukesh, unaweza kutumia usafiri wa aina mbalimbali. Kama unajua wazi kwamba foleni za India zitakufanya uwe unasonya njia nzima basi unaweza kuchukua helikopta, pale nyumbani kwa bwana Mukesh kuna viwanja vitatu kwa ajili ya usafiri huo. Kama namna gani vipi umenunua gari mpya na unataka kwenda nayo kumlingishia bwana Mukesh usitie shaka, ana uwanja wa kuegesha magari 160 kwa wakati mmoja.
Ukishuka kwenye gari au kipepeo (helikopta) chako kuna lifti tisa zinakusubiri wewe uende kokote katika ghorofa hizi 27, kwa hiyo dada zangu msitie shaka, komeleeni michuchumio ile ile ya mwaka.
Habari na http://www.fotobaraza.me/

0 comments:
Post a Comment