Dk Wilbrod Slaa Apagawisha Bukoba
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA)Dk.Willibrod Slaa,akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa
Bukoba na vitongoji vyake,katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa
Uhuru janaMgombea
urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dk.Willibrod
Slaa,akiwapungia mkono wakazi wa mji wa Bukoba, akiwa katika msafara
kuelekea katika Uwanja wa Uhuru mjini humo,ambako alifanya mnkutano wa
kampeni .
Na Mwandishi Wetu, Kibondo, Kigoma
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Dk. Willbroad Slaa (pichani) amewataka wafuasi wa chama chake kutolipiza kisasi wanapofanyiwa fujo na wanachama au wafuasi wa vyama vingine.
Akihutubia katika mkutano wa kampeni, mjini hapa juzi kati, Dk. Slaa aliwataka wana Chadema kuwa wa mwisho kuanzisha vurugu kabla na baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchi nzima Oktoba 31, mwaka huu.
“Chadema haitakubali kuona wanachama na wafuasi wake wakianzisha vurugu, hata kama mkichokozwa msilipe kisasi kwani CCM itapata kisingizio,” alisema Dk. Slaa.
Aidha, alimtaka mgombea Urais mwenzake wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuacha kuhubiri amani kama hatakifuta kikundi cha Green Guard ambacho alidai wamekuwa chanzo cha kuvuruga amani sehemu mbalimbali nchini.
Katika mkutano huo, Mbunge anayemaliza muda wake wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alitangaza majimbo ambayo Chadema inaamini itazoa ushindi katika M-koa wa Kigoma kuwa ni Manyovu, Kigoma Kaskazini, Mhambwe na Kigoma mjini.

0 comments:
Post a Comment