Burundi, Congo kati ya nchi zilizoathiriwa zaidi na njaa na umaskini duniani
Taasisi ya Kimataifa ya Kuchunguza Sera za Chakula IFPRI imetangaza katika ripoti yake mpya kwamba idadi ya watu wanaosumbuliwa na njaa katika mwaka huu wa 2010 imefikia bilioni moja. Taasisi ya IFPRI imetangaza kuwa kiwango cha umaskini na njaa katika nchi 25 kati ya nchi 122 zilizohusishwa katika uchunguzi huo kimefikia awamu ya hatari kubwa.
Ripori ya International Food Policy Research Institute kuhusu nchi zilizoathiriwa mno na njaa na umaskini imejumuisha nchi nne za Afrika ambazo ni Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Eritrea na Chad.
Ripoti hiyo imesisitiza kuwa umaskini, machafuko na ghasia za kisiasa ni miongoni mwa sababu kuu za matatizo hayo ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment