SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, August 1, 2010


FIESTA JIPANGUSE 2010 NDANI YA YATCH CLUB USIKU WA KUAMKIA LEO.

Wasanii AT pamoja na Ray C wakiimba wimbo wao ya mama ntilie mbele ya wakazi wa Mwanza waliojitokeza usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 ndani ya Yatch Club.
Msanii Diamond (kati) na densa wake wakiukumbuka mzimu wa Michael Jakson usiku wa kuamkia leo ndani ya ya Yatch Club
Msanii Beatrice amabye pia ni mkazi wa jiji la Mwanza akiwakuna vilivyo wenyeji wake.
Watu kibao waliofurika ndani ya Yatch Club usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Fiesta jipanguse 2010,ambali mdhamini wake mkuu ni kampuni ya bia ya Serengeti.
Mkali mwingine anaefanya mziki kama hobi na si kazi, Ncha Kali (kulia) wakikamu vilivyo na mkali wa hip hop hapa bongo Fid Q.
Wanaume Halisi,Juma Nature na Dolo wakiamsha mzuka wa kutosha kwa wakazi wa Mwanza waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta jipanguse 2010 ndani ya Yatch Club usiku wa kuamkia leo.
Wakazi wa mwanza wakijipangusa kwa raha zao huku mfalme wa raha kamili tayari amekwisha dumu zaidi vichwani mwao.
Mwamba wa kazi kazini Joe Makini akiangusha mistari yake migumu ya kihip hop mbele ya umati mkubwa uliofika kwenye tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya Yatch Club.
Rehema Chalamila a.k.a Ray C kiuno bila mfupa akionesha umabiri wake wa kuchezea kiuno chake jukwaani.Kwa hakiksa Ray C bado yuko fiti kabisa.
Wazee wa Bata kutoka zenji mpaka kanda ya Ziwa jijini Mwanza,Offside Trick wakiimba bila bata wa Mwanza.!
Barnaba na Lina wakiwaimbia washabiki wao wimbo wao wa Kisa Meseji ambao umekuwa ukifanya vizuri na kupendwa zaidi na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya.
Kutoka kundi la Wanaume TMK,Chege na Themba wakiwakilisha vyema usiku wa kuamkia leo ndani ya Yatch Club.
Mfalme wa Raha Kamili kama kawaida yake alikuwepo kila mahali kuhakikisha wakazi wa mwanza raha yao inadumu zaidi kila wakati.
Mwasiti akiwaimbisha washiki wake singo mpya ya kisa pombe ambayo imeonekana kukubalika kwa kiasi kikubwa,kiasi kwamba hata yeye awapo jukwaani hujituma vilivyo.
Lina akimpagawasiha mkazi wa Mwanza na wimbo wake wa atatamani .!

Chui chui wakiangusha moja ya bonge la shoo aina ya kiduku jukwaani ndani ya Yatch Club usiku wa kuamkia leo.Tamasha la Fiesta Jipanguse leo nchana litakuwepo ndani ya CCM Kirumba kwa kiingilio cha shilingi 2500/= kwa kila kichwa,kama vipi rrrhhhhhaaaa si ya kuikosa tena mtu wangu.

0 comments:

Post a Comment