Nigeria 'yasalimu amri kwa Fifa'
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Nigeria, serikali ya
nchi hiyo imebatilisha uamuzi wake wa kuizuia timu ya soka ya taifa ya
nchi hiyo kushiriki mashindano yote ya kimataifa.
Taarifa hizo zimetolewa saa moja kabla ya
kufikia muda wa mwisho uliowekwa na shirikisho la soka duniani Fifa la
kubatilisha uamuzi huo.
Fifa ilisema itaifungia Nigeria kushiriki
mashindano ya soka duniani iwapo serikali ingeonekana kuingilia.
Wiki iliyopita Rais Goodluck Jonathan alisema
baada ya timu hiyo kuonyesha kiwango duni katika Kombe la Dunia watazuia
kushiriki mashindano yeyote ya soka kwa miaka miwili.
Siku ya Jumapili, maafisa waandamizi wawili wa
shirikisho la soka la Nigeria (NFF) walifukuzwa katika hatua ya
kumtuliza Rais huyo.
Chanzo cha habari kimeiambia BBC kuwa kufukuzwa
kwao hakujabadili uamuzi wa Rais huyo, lakini NFF liliomba kuzungumza
naye Jumatatu kwa mazungumzo ya dharura kabla ya siku hiyo waliopewa na
Fifa kuwadia.
0 comments:
Post a Comment