SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, July 6, 2010

Mawaziri kujadili mishahara ya wabunge
Rais Mwai Kibaki
Rais Mwai Kibaki
Rais wa Kenya, Mwai Kibaki baadaye leo asubuhi anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kujadili pendekezo la wabunge wa nchi hiyo la kujiongezea mishahara na kuwa miongoni mwa wabunge wanaolipwaa kiasi kikubwa zaidi cha mshahara duniani.
Ikiwa pendekezo hilo litaidhinishwa na rais Kibaki kuwa sheria, wabunge hao watapokea dola lefu mia moja hamsini kila mwaka kama mishahara.
Lakini viongozi wakuu wa serikali akiwemo Waziri Mkuu Raila Odinga wamepinga pendekezo hilo. Bw. Odinga amesema pendekezo hilo la wabunge, limetolewa wakati mbaya ambao wakenya wanakabiliwa na changamoto nyingi.
Mkenya akipelekwa hopsitalini
Mkenya akipelekwa hopsitalini
Vyama vya wafanya kazi pia vimetishia kuongoza mgomo ikiwa rais Kibaki ataidhinisha pendekezo hilo kuwa sheria.
Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini humo, Francis Atwoli, amesema ni aibu kwa wabunge hao kupitisha mswada wa kuongeza mishahara yao, ili hali walipinga mswada uliowashinikiza wabunge hao kulipa ushuru.
***********************
Rais wa Brazil awasili Kenya katika mfululizo wa ziara yake Afrika
Sample Image Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil amewasili nchini Kenya kwa ajili ya ziara rasmi. Habari zinasema kuwa, ziara hiyo inalenga kustawisha uhusiano wa kibiashara na uwezekazaji baina ya pande mbili.
Lula da Silva ni Rais wa kwanza wa Amerika ya Latini kutembelea Afrika Mashariki na amepangiwa kukutana na Rais Mwai Kibaki leo Jumanne.
Inatarajiwa kuwa mazungumzo ya Marais wa nchi hizo mbili yatalenga kwenye sekta za kilimo, nishati, miundombinu, sayansi na teknolojia.
Uhusiano kati ya Kenya na Brazil unazidi kustawi siku baada ya siku tangu Nairobi ilipofungua ubalozi wake nchini Brazil mwaka 2008.
Kabla ya hapo Rais wa Brazil alikuwa ameshiriki katika kikao cha ECOWAS kilichofanyika nchini Cape Verde siku ya Jumamosi.
Siku ya Jumapili alitembelea Equatorial Guinea na kuonana na Rais Teodoro Obiang Nguema wa nchi hiyo.
Akitoka Kenya Rais huyo wa Brazil atatembelea nchi za Tanzania, Zambia na Afrika Kusini ambako atashuhudia mechi ya fainali ya Kombe la Dunia la Mpira wa Miguu mwaka huu inayotarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili ya Julai 11.

0 comments:

Post a Comment