Watu
wasiopunga 11 wameuawa leo nchini Somalia katika mapigano yaliyozuka
baada ya wanamgambo wa Al Shabab kushambulia kituo cha vikosi vya
serikali kusini mwa mji mkuu Mogadishu. Ahmed Warsamae, afisa usalama wa
serikali amesema kwamba, mapigano hayo yalianza leo asubuhi baada ya
kituo chao kilichoko karibu na eneo la Hosh kushambuliwa na wanamgambo
wa Al Shabab na kupelekea watu watatu kuuawa. Ameongeza kuwa, baada ya
shambulizi hilo nao pia waliwashambulia vikali wanamgambo hao na kwamba
watu wasiopungua 8 waliuawa katika tukio hilo. Wanamgambo wa Al
Shabab wanadhibiti theluthi mbili ya ardhi ya Somalia na wamekuwa
wakifanya mashambulizi na kukaribia pambizoni mwa mji mkuu Mogadishu,
ulioko chini ya udhibiti wa serikali ya mpito inayoungwa mkono na nchi
za Magharibi na kusaidiwa na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa
Afrika.
Serikali ya Uganda kuwalipa fidia waliolemazwa na waasi wa
LRA kabla ya uchaguzi |
|
|
|
Serikali ya
Uganda itawalipa fidia watu wapatao 10,000 wa eneo la kaskazini mwa nchi
hiyo waliolemazwa na waasi wa LRA, kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa
nchi hiyo mwakani. Richard Todwong Mshauri Maalum wa Rais Yoweri
Museveni wa eneo la Kaskazini mwa Uganda amesema leo kuwa, serikali
imeanza kuorodhesha kila mtu aliyelemazwa au kusababishiwa matatizo ya
kimwili na waasi wa LRA, ili kutayarisha orodha ya wahanga watakaopewa
fidia. Ameongeza kuwa, licha ya kuwa wananchi wote wa kaskazini mwa
Uganda walipata mateso au madhara kwa njia moja au nyingine kutokana na
vitendo vya waasi hao, lakini kwa sasa wanawatafuta na kuwaorodhesha
wale waliopata ulemavu au aina nyinginezo za madhara ya kimwili. Mwezi
Februari serikali ya Uganda pia ilianzisha mpango wa dola milioni 100 wa
ukarabati ili kuhuisha tena miundo mbinu ya kiuchumi na kijamii
iliyoharibiwa na vita vya ndani, kabla ya uchaguzi mkuu wa rais na bunge
unaotarajiwa kufanyika mwezi Februari mwaka ujao. Waasi wa kundi la
Lord's Resistance Army (LRA) linalotaka kusimamisha sheria 10 za
Kikirsto nchini Uganda ni maarufu kwa kuua raia na kuwateka nyara
wanawake na watoto na kuwatumia katika vitendo vya ngono, kuwatumikisha
watoto vitani na kukata viungo mbalimbali vya wale wanaowakamata.
|
|
0 comments:
Post a Comment