Uchunguzi wa
maoni uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kwamba wananchi wa Marekani
wamepoteza imani na utendaji kazi wa Rais Barack Obama baada ya serikali
yake kushindwa kuziba kisima cha mafuta katika Ghuba ya Mexico. Kwa
mujibu wa uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na kanali ya televisheni ya
CNN, karibu zaidi ya nusu ya Wamarekani wanaamini kuwa, Obama hana
uwezo wa kutosha wa kushughulikia matatizo yanayoikabili nchi hiyo na
wananchi wake.
Uchunguzi huo aidha umeeleza kwamba, mtazamo wa watu wengi wa Marekani ni kwamba kushindwa Obama kutatua mgogoro wa kuvuja mafuta katika kisima cha shirika la Uingereza la British Petroleum BP huko baharini ni sawa na kushindwa George Bush rais wa zamani wa Marekani kushughulikia matatizo ya tufani ya Katrina. Hii ni katika hali ambayo Mkuu wa Shirika la Mafuta la Uingeza BP amejigamba kuwa shirika hilo bado ni imara hata kama limekumbwa na matatizo kutokana na kisima chake cha mafuta kuvuja kwenye Ghuba ya Mexico.Carl Henric Svanberg pia amekanusha matamshi ya Rais wa Russia kwamba shirika hilo linaweza kusambaratika
Mbunge mmoja wa Ujerumani ataka uhusiano wa nchi hiyo na Israel uvunjwe
Kiongozi wa chama cha Ujerumani cha National Democratic Party (NDP)
ameitaka nchi hiyo ivunje uhusiano wa aina yoyote ile na utawala wa
Kizayuni wa Israel na pia ametaka utawala huo ghasibu uwekewe vikwazo
vya kiuchumi.
Holger Apfel amesema katika hotuba yake iliyozusha mjadala mkubwa kwenye Bunge la Ujerumani kwamba, inabidi uhusiano na Wazayuni makatili wa Israel uvunjwe mara moja na haipaswi kuunga mkono ngano zisizo na ukweli za Holocaust. Mbunge Apfel pia alikataa kuondoka jukwaani baada ya muda wake kuisha, na alipoondolewa kwa nguvu aliendelea kuwaita Wazayuni kuwa ni magaidi. Kwa upande mwingine Bunge la Umoja wa Ulaya limepitisha azimio dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Azimio hilo linataka kufanyike uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu jinai zilizofanywa na makomandoo wa Israel dhidi ya msafara wa meli zilizokuwa zinaelekea Ghaza zikiwa na misaada ya kibinaadamu. Swahili Radio . Hali bado tete nchini Kirgistan
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa
, Ban Ki-moon ametoa wito kwa mataifa wanachama wa umoja huo
kuchangia misaada ya kiasi cha euro milioni 58 kwa ajili ya
nchi ya Kirgistan
Waandamanaji
wanajikusanya mbele ya jengo la serikali
wakizuiwa na polisi katika mji wa Talas, nchini Kyrgyzstan.
NEW YORK:
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Ban Ki-moon ametoa mwito kwa
wanachama wa umoja huo kuchanga msaada wa kiasi cha Euro milioni 58 kwa
ajili ya nchi ya Kyrgyzstan iliyokumbwa na machafuko ya kikabila. Ban
ki-moon amesema fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia kiasi ya wakimbizi
300,000 na raia wengine walioathirika kwa machafuko hayo.
Hapo awali,Rais wa mpito wa
Kyrgyzstan, Rosa Otubajewa alikiri kuwa
idadi ya watu waliouawa huenda ikawa ni 2,000 - hiyo ni mara kumi zaidi
ya vile ilivyotathminiwa hapo awali. Wakati huo huo Urusi inafikiria
kupeleka wanajeshi wake nchini Kyrgyzstan ili kulinda vituo muhimu
nchini humo. Lakini uamuzi bado haujapitishwa. Hiyo ni kwa mujibu wa
vyombo vya habari vya Urusi vilivyoinukulu wizara ya ulinzi mjini
Moscow.
|
Saturday, June 19, 2010
Wananchi wa Marekani hawana imani na Rais Barack Obama
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, June 19, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment