SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, June 1, 2010

Rais wa Ujerumani ajiuzulu

Rais Horst Koehler wa Ujerumani ametangaza kujiuzulu

Rais Koehler amechukua hatua hiyo kutokana na kauli aliyoitoa kuhusiana na harakati za majeshi ya Ujerumani nchini Afghanistan.
Koehler akiwa katika ziara ya kushtukiza nchini Afghanistan hivi karibuni, alisema kuwa majeshi ya Ujerumani yako nchini humo kwa maslahi ya kiuchumi zaidi.
Hii ni mara ya kwanza tokea kumalizika kwa vita vya pili vya dunia kwa rais wa Ujerumani kujiuzulu.
Spika wa Bunge la Ujerumani Bundestag Jens Boehrnsen sasa anawajibika kumteua mtu wa kujaza nafasi hiyo.
Horst Koehler mwenye umri wa miaka 67  kutoka chama cha Kansela Angela Merkel cha CDU amekuwa katika nafasi hiyo ya urais tangu Julai 2004.
Mwaka jana alichaguliwa tena kushika wadhifa huo . Aliwahi kuwa waziri mdogo katika wizara ya fedha chini ya  Waziri Theo-Waigel wakati wa utawala wa  Kansela Helmut Kohl kabla ya  kuwa Mkurugenzii Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF mwaka 2000.
Alikatiza kipindi chake kuwania  Urais wa Ujerumani baada ya kuteuliwa na chama chake cha CDU akiungwa mkono na CSU na FDP na kumrithi mtangulizi wake Johannes Rau kutoka chama cha SPD.
Mwandishi:Aboubakary Liongo/DPA
Mhariri:Mohamed Abdulrahman

0 comments:

Post a Comment