Makao makuu ya kanisa la
Kikatoliki Vatican imekubali hatua ya kujiuzulu kwa askofu wa Ireland
aliyekuwa Nigeria kutokana na shutuma za kumdhalilisha kijinsia binti
mmoja huko Niger Delta.
Richard Burke, askofu wa mji wa Benin, amekubali
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti huyo lakini amekana kwa binti
huyo kuwa na umri mdogo uhusiano huo ulipoanza.
Katika taarifa iliyotolewa kwenye gazeti la
kikatoliki la Ireland amesema, " Sababu ya kujiuzulu ni kutokuwa
mwaminifu katika kiapo changu cha useja."
Askofu huyo amejiuzulu baada ya madai hayo
kutolewa mwaka jana.
Dolores Atwood alidai kunyanyaswa kijinsia na
askofu Burke wakati alipokuwa padri huko Warri kusini mwa Nigera kwenye
mji wa Niger Delta.
Hata hivyo, amesema uhusiano wao ulianza mwaka
1989 alipokuwa miaka 40 na binti akiwa na umri wa miaka 21.
Amesema kwenye taarifa yake, " Nilijibu haraka
iwezekanavyo kwamba sijawahi hata siku moja maishani mwangu kumnyanyasa
mtoto kijinsia. Huu bado ni msimamo wangu. Huu ni ukweli."
Askofu Burke pia alimwomba radhi Bi Atwood na
kuomba msamaha katika vituo vyake vya kanisa huko Warri na Benin.
Kanisa hilo limesema limekubali kujiuzulu kwake
ambapo pia limetaja jopo litakalochunguza udhalilishaji wa watoto
uliofanywa na viongozi wa kikatoliki huko Ireland.
uliofanywa na viongozi wa kikatoliki huko Ireland.
0 comments:
Post a Comment