England na Algeria zilitoka sare
0-0 siku ya Ijumaa katika mechi ya kundi la C kwenye michuano ya Kombe
la Dunia mjini Cape Town, matokeo yaliyoiweka England katika hatari ya
kuyaaga mashindano mapema kuliko ilivyotarajiwa. Wayne Rooney
akidhibitiwa vilivyo na wachezaji wa Algeria
Ili kufuzu kwa raundi ya pili ni lazima England
ipate ushindi mkubwa katika mechi inayofuata dhidi ya Slovenia, ambayo
ilitoka sare na Marekani 2-2.Slovenia sasa inaongoza kundi hilo la C ikiwa na
pointi 4 kutokana na mechi 2, baada ya kuishindia Algeria 1-0 katika
mechi ya kwanza, na baada ya kutoka sare 2-2 na Marekani.Marekani ina pointi mbili sawa na england lakini
Marekani iko mbele kwa wingi wa mabao; nayo Algeria ina pointi moja
kutokana na sare ya Ijumaa.Wachezaji wa England walizomewa na mashabiki wao
baada ya mechi hiyo iliyodhibitiwa zaidi na Algeria.
Mabadiliko
Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney,
alionekana mdhaifu muda wote wa mechi hiyo ingawa kocha Fabio Capello
alifanya mabadiliko kuwaondoa Emile Heskey, Gareth Barry na Aaron Lennon
ambao nafasi zao zilichukuliwa na Shaun Wright-Philips, Jermain Defoe
na Peter Crouch. Kutokana na mabadiliko hayo Jermain Defoe
aliisumbua mara kadhaa safu ya ulinzi ya Algeria lakini bila mafanikio
ya kutikisa nyavu. Capello alikuwa amempumzisha mlinda lango Robert
Green ambaye katika mechi ya kwanza alilaumiwa kwa kosa lililoipa
Marekani bao la kusawazisha,na nafasi hiyo kuchukuliwa na David James.Kocha wa Algeria Rabah Saadane naye pia
alimpumzisha kipa Fawzi Chaouchi ambaye vile vile alifanya kosa katika
mechi ya ufunguzi lililowapa ushindi Slovenia na kumchezesha Rais
M'Bolhi.
Wasiwasi
Rooney alitazamiwa kuwa miongoni mwa wachezaji
bora kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010, lakini katika
mchezo wa Ijumaa wazo hilo lilionekana kama dhana isiyokubalika. Badala ya Rooney, kiungo wa Algeria Karim Ziani
anayeichezea klabu ya Wolfsburg ndiye aliyeonekana kutia fora zaidi. Mlinzi Jamie Carragher alipata kadi ya pili ya
njano baada ya kumchezea visivyo Hassan Yebda, na atakosa mechi
inayofuata.
0 comments:
Post a Comment