SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 1, 2010

Ngorongoro Heroes yaitungua Malawi 3-1 na kufuzu kucheza kombe la mataifa ya afrika kwa vijana


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes , Thomas Ulimwengu (kulia) akimtoka beki wa timu ya vijana ya Malawi, Lucky Malata (5) katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Ngorongoro ilishinda 3-1. Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes , Thomas Ulimwengu (kulia) akiwania mpira sambamba na beki wa timu ya vijana ya Malawi, Limbikani Mzava katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Ngorongoro ilishinda 3-1. Golikipa wa timu ya taifa ya Malawi ya vijana chini ya miaka 20, Alex Makina akiuangalia mpira ukitinga wavuni na kuhesabu bao la pili kwa timu ya taifa ya Ngorongoro Heroes. kocha wa timu ya taifa ya vijana ya Malawi akiwa ameeduwaa baada ya mchezo kumalizika
Kocha wa timu ya vijana chini ya 20, Rodrigo Stockler akimpongeza mfungaji wa bao la pili la timu hiyo, Omega Seme wakati mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Ngorongoro ilishinda 3-1. Kwa matokeo hayo timu ya ngorongoro itakutana na timu ya vijana ya Ivory Coast wiki ya tatu ya mwezi mei ambapo mchezo wa kwanza utafanyika katika nchini Ivory Coast na baada ya wiki mbili timu hizo zitarudiana katika dimba uwanja wa taifa, Dar es Salaam.
wachezaji wa timu za Tanzania na Malawi wakiomba dua kwa pamoja mara baada ya mchezo kumalizika.
Mashabiki walioingia bure kuipa sapoti NgorongoroHeroes
 

0 comments:

Post a Comment