Mwanamziki mkongwe
wa mziki wa dansi nchini toka nchini Kongo Kinshasa, Fredy Mayaula
Mayoni (RIP) amefariki dunia siku ya 27-05-2010 huko jijini Brussels,
Ubeligiji, kwa ugonjwa kansa ya ubongo (brain trumour).
Marehem Mayaula Mayoni (64) ni mwanamziki aliyekulia na kusomea jijini Dar wakati wa utoto wake miaka ya 60s, kwani baba yake alikuwa ni moja wanadiplomasia katika ubalozi wa Kongo(Zaire) nchini Tanzania. Marehem pia aliwahi kucheza kandanda katika timu maarufu nchini Yanga(Young Africa) ya jijini Dar.
Vijana wa kizamani watamkumbuka marehemu Mayaula pale alipojiunga na bendi ya TP OK Jazz,iliyokuwa inaongozwa na gwiji Franco Luambo Makiadi, uko Kongo. Mayaula alijiunga TP OK Jazz baada ya kurudi kwao Kongo (DRC) na kujikita katika ulimwengu wa mziki ,ambako aliachia wimbo maarufu "Cherie Bondowe" au "Sherry bondowe", wimbo ambao ulimpa umaarufu sana.marehemu pia aliwahi kufanya kazi na mwanamziki ambaye pia marehemu Mpongo Love.
Mungu amlaze pema peponi Mayaula Mayoni
Amin
0 comments:
Post a Comment