ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A LOWEST COST AND ALSO SEND TO US NEWS, EVENTS FOR MORE INFORMATION CONTACT US TELEPHONE: +919160901191 E-mail: ally.shaaban@yahoo.com | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU NA PIA TUTUMIE HABARI, MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +919160901191 Barua Pepe: ally.shaaban@yahoo.com | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI HAPA

Thursday, September 30, 2010

GENEVIEVE AKABITHIWA BENDERA YA TAIFA
Genevive Emmanuel akiwa ameshikilia bendera ya taifa mara baada ya kukabidhiwaa rasmi tayari kwa safari yake ya kuelekea nchini China leo. Vodacom Miss Tanzania, Genevieve Emmanuel Mpangala,jana alikabithiwa Bendera ya Taifa tayari kwa safari yake ya kuelekea nchini China katika jiji la Sanya ambako shindano la dunia Miss World 2010 linatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu. Genevieve ataondoka leo kwa ndege ya Shirika la Quatar Airways akipitia Uarabuni, Mongolia na kisha Sanya nchini China. 
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi na aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi bendera ya taifa kwa Vodacom Miss Tanzania 2010, Esther Mkwizu (wa pili kushoto) akikabidhi bendera hiyo huku wazazi wa Genevive wakishuhudia, kulia ni baba yake Bw. Emmanuel Mpangala na kushoto ni mama yake Mary.
Mwana wa kiume wa Gaddafi aikosoa vikali serikali ya baba yake

Sample Image
Mwana wa kiume wa kiongozi wa Libya Saiful Islam Gaddafi ameikosoa vikali serikali ya nchi hiyo akisema kuwa haina uwezo wa kuendesha nchi. Saiful Islam ambaye anatazamwa kama mrithi wa Kanali Gaddafi katika uongozi wa Libya ameishambulia serikali ya nchi hiyo baada ya kutembelea chumba cha nchi hiyo katika maonyesho ya kimataifa ya Shanghai huko Uchina. Amesema serikali ya Tripoli haikuchukua hatua za maana za kushughulikia chumba cha Libya katika maonyesho hayo ya kimataifa akisema hakuna serikali nchini Libya.
Matamshi hayo ya Saiful Islam Gaddafi yanaakisi migawanyiko inayotawala safu za watawala wa Libya na ushindani mkubwa wa kuwania madaraka uliopo kati ya kambi ya mwanasiasa huyo kijana inayotaka marekebisho na ile ya wazee na wasaidizi wa baba yake.
Wachambuzi wanasema Saiful Islam ndiye nayeonekana kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuongoza Libya baada ya baba yake Muammar Gaddafi lakini atalazimika kwanza kuwabwaga wahafidhina katika serikali, jeshi la Libya na vyombo vya upelelezi vya nchi hiyo.
Benki kuu ya Kenya kuchunguza "Hawala"
Kenya imetangaza mipango inayonuia kudhibiti ufadhili wa kifedha unaotolewa kwa wapiganaji wa kiisilamu wa Al- Shabaab nchini Somalia.
Benki Kuu ya Kenya imeziagiza benki zote nchini kuchunguza shughuli za kibiashara zinazohusishwa na wafanyibiashara walioorodheshwa kama wafadhili wa ugaidi na Umoja wa Mataifa.
Hatua ya Kenya katika kujaribu, kupunguza nguvu za wanamgambo wa Ki-Somali inatokea wiki moja baada ya baraza la usalama la umoja wa Mataifa kufanya kikao maalum kilichoangazia hali ya Somalia.
Wadadisi wa mambo ya usalama wamekuwa wakisisitiza kwamba Nairobi imekuwa kivukishio cha ufadhili wa makundi yanayokabiliana na serikali ya mpito ya somalia.
Moja ya njia zinazotumiwa na wasomali kuwatumia jamaa zao fedha ni Hawala.

Wednesday, September 29, 2010

Kiongozi wa NK anuia kumpokeza mwanaye


Mtoto wa kiume wa mwisho wa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-il, ameteuliwa katika nyadhifa mbili za juu nchini humo. Kijana huyo Kim Jong-un aliye na chini ya miaka 30 hajawahi kuhudumu katika afisi yoyote ya umma nchini humo na hatua ya kumteua inaonekana kuwa maandalizi yake kuchukuwa wadhifa wa baba yake kama kiongozi wa nchi.
Uongozi wa Korea Kaskazini
Kuchambua uongozi wa Korea Kaskakazini wenye usiri mwingi sio kazi rahisi, lakini inaonekana wazi kuwa Kim Jong-Un sasa ameteuliwa kuchukua uongozi wa nchi hiyo.
Hii inashiria mwanzo wa kipindi cha mpito ambacho muda wake bado haujajulikana.
Babake, Kim Jong-Un anaugua na inaaminika kuwa alipooza mara mbili , mwaka wa 2008. Uamuzi wake wa kuanzisha kipindi hiki cha mpito ni ishara kwamba hali yake ni mbaya.
Kim Jong - Un ni nani?
Machache yanajulikana kuhusu Kim Jong-Un tangu wakati alipokuwa akisomea nchini Uswizi. Hata umri wake haujulikani na inadhaniwa kuwa ana umri wa miaka 27.
Hali ya wasiwasi inazingira mipango ya kumrithi Kim Jong-Il. Huenda Kiongozi huyo wa kikomunisti akaondoka madarakani polepole au huenda kiongozi mwenye ushawishi ,mwenye cheo cha tatu cha juu katika utawala huo, Jang Song-Thaek, ambaye pia ni mwenyekiti wa tume kuu ya kitaifa ya ulinzi, akafanywa kuwa mshauri wa kijana Kim Jong-Un?
Swali lingine ni kuhusu shughuli ya kumuandaa kijana Un. Je! itachukua muda gani kabla ya yeye hatimaye kushikilia wadhifa huo?
Hii ndio sababu waangalizi wa nje wa masuala ya Korea Kaskazini wana wasiwasi sana.
Korea Kaskazini bado inatawaliwa kijeshi. Kama kutafanyika mabadiliko machache katika tume kuu ya jeshi la nchi hiyo, basi huenda uhusiano na nchi za nje usibadilike.

RATIBA LIGI YA MABINGWA ULAYA LEO

LIGI YA MABINGWA ULAYA:
LEO JUMATANO 
R.kazan Saa 1:30 Barcelona 
 Tottenham 3:45 FC Twente 
Inter    Milan 3:45 W.Bremen
 Schalke 3:45 Benfica 
Hapoel 3:45 Lyon 
 Rangers 3:45 Bursaspor 
Valencia 3:45 Man Utd  
Panathinaik 3:45 Copenhagen


Rooney kutocheza mechi ya Valencia:


Wayne Rooney


Wayne Rooney

Wayne Rooney hatasafiri na kikosi cha timu yake ya Manchester United siku ya Jumatano kwa ajili ya mchezo ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Valencia, kutokana na kuumia kiwiko cha mguu.


Manchester United ilikuwa na matumaini mshambuliaji huyo atakuwa imara kucheza mechi hiyo katika uwanja wa Mestalla.
Lakini Rooney aliyebadilishwa siku ya Jumapili Man United walipotoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Bolton, sasa ameungana na Ryan Giggs katika orodha ya majeruhi.
Giggs anakabiliwa na maumivu ya paja, hali itakayomfanya asicheze soka kwa wiki mbili zijazo.
Meneja msaidiza wa Man United Mike Phelan alisema baada ya mechi na Bolton Rooney angekuwa tayari kwa ajili ya pambano la ligi ya Mabingwa wa Ulaya, lakini vipimo alivyofanyiwa vimeonesha hawezi kucheza.
Manchester United ambao walianza heka heka za ligi ya Mabingwa wa Ulaya katika kundi lao la C kwa kwenda sare ya kutofungana na Rangers, itaikabili Valencia ambayo kwa sasa inaongoza ligi ya Hispania.
Valencia walianza kampeni ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa kuichakaza Bursaspor ya Uturuki mabao 

4-0.
Msimu huu Rooney bado hajaonesha makali, hali iliyomfanya meneja wake Sir Alex Ferguson akiri mchezaji wake huyo hajisikii vizuri kutokana na kuandikwa na kutangazwa sana na vyombo vya habari baada ya tuhuma zilizohusu maisha yake binafsi.

P-FUNKY AELEZEA MADAI YA AFANDE SELE KUTOLEWA BASTOLA!

Producer na mmiliki wa Bongo Records, P.Funky 'majani', ambaye wikiendi iliyopita aliingia katika 'bifu' na Mfalme wa Rhymes Afande Sele, amevunja ukimya na kuongelea tukio hilo. Majani anakiri kumchapa kibao Afande lakini anakanusha kumtolea bastola kama alivyodai Sele na kunukuliwa katika media, Hapa anaelezea kisa kizima na sababu zilizomfanya amuadabishe mfalme huyo wa Rhymes wa Bongo...Bonyeza player msikilize mwenyewe.......
Producer P- Funky 'Majani'
PICHA/VIDEO: Mussa Mateja

Tuesday, September 28, 2010

Mahakama Yatoa Amri Mzee Andrew Chenge Akamatwe Haraka

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge
Bajaj iliyogongwa Machi 27, 2007
Gari la Chenge baada ya ajali Machi 27, 2007
------------
BAADA ya kutoonekana mahakamani jana , Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kinondoni, Dar es Salaam imeamuru kukamatwa kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.
Chenge ambaye yuko nje kwa dhamana akikabiliwa na mashitaka ya kusababisha vifo vya watu wawili, jana hakufika mahakamani hapo wala mdhamini wake bila taarifa.
Amri hiyo ilitolewa mahakamani hapo na Hakimu Sundi Fimbo, baada ya mwendesha mashitaka, Richard Rweyongeza kusoma maelezo ya awali ya mashitaka yanayomkabili mshitakiwa.
“Haijalishi kuwa mshitakiwa yuko kwenye kampeni au wapi, Mahakama haitambui jambo lolote kuhusu kampeni, hivyo kwa kuwa hajahudhuria mahali hapa, inabidi akamatwe kwa kushindwa kutekeleza amri ya Mahakama,” alisema Hakimu Fimbo.
Alifikia uamuzi huo baada ya masharti ya dhamana ambayo yanamtaka mshitakiwa kufika mahakamani siku ya kesi aliyopangiwa na bila hivyo atoe taarifa za kutofika kwake mahakamani.
Kwa niaba ya Hakimu Mkazi, Kwey Rusema, ambaye anasikiliza kesi hiyo, Hakimu Fimbo aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 5 mwaka huu itakaposikilizwa tena.
Ilidaiwa kuwa Machi 27, 2007 mshitakiwa akiendesha gari aina ya Toyota Hilux namba T 512 ACE alimgonga mwendesha pikipiki ya magurudumu matatu - bajaj jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya Beatrice Costantine na Victoria George.
Awali baada ya Mahakama kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka, Mahakama ilisema Chenge ana kesi ya kujibu na alitakiwa kufika mahakamani jana kuanza kusikiliza utetezi wake.
Chenge ambaye anatetea ubunge Bariadi Magharibi alisema ataleta mashahidi wawili ambao ni yeye na shahidi mwingine ambaye hakutajwa mahakamani.
Aidha, katika kesi hiyo shahidi wa mwisho wa upande wa mashitaka, Raymond Njeje, alidai kuwa stika ya bima aliyokuwa akitumia Chenge si mali yake.
Njeje alidai kuwa, stika hiyo ni ya gari namba T 571 AKH aina ya Toyota RAV4 nyeusi na si ya Toyota Hilux iliyosajiliwa kwa namba T 513 ACE ambalo alikuwa akiendesha Chenge wakati anapata ajali.
Alidai stika hiyo namba 11919156 inamilikiwa na Evarist Ses iliyotolewa mwaka 2007 kwa ajili ya matumizi ya miezi mitatu kuanzia Juni 29 hadi Septemba 28.
Gazeti hili lilimtafuta Chenge kwa njia ya simu jana akasema kuwa hayuko tayari kuzungumza chochote kwa sasa kuhusu kesi ambayo ipo mahakamani.
Mgaya Kingoba, anaripoti kutoka Bariadi kwamba Chenge alikuwa katika kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete zilizofanyika Bariadi Mashariki mkoani Shinyanga.
 
Katika kampeni hizo, Chenge ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM alikuwa akizungumza akichanganya Kiswahili na Kisukuma, akiwataka wakazi wa jimbo hilo kutofanya makosa tena, akitolea mfano wa mazuri yaliyofanywa na chama hicho jimboni mwake.
Alikuwa akimnadi mgombea ubunge wa CCM katika jimbo la Bariadi Mashariki, Martin Makondo baada ya Rais Kikwete kumaliza kumnadi.
Mapema katika mkutano huo, Kikwete aliwaambia wananchi wa Bariadi Mashariki, kwamba miaka 15 waliyochagua Mbunge wa upinzani inatosha na sasa wakipe chama hicho nafasi ya kuongoza Halmashauri yao na wataona mabadiliko makubwa zaidi.
Alisema chini ya falsafa ya Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi, wananchi hao wana kila sababu ya kuichagua CCM kuongoza jimbo hilo na wataona tofauti na walivyokuwa na mbunge wa mpinzani.
Bariadi Mashariki imekuwa chini ya UDP, kuanzia mwaka 1995; kwanza chini ya Danhi Makanga ambaye baadaye aliihama na kujiunga na CCM na sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo na sasa linaongozwa na John Cheyo, Mwenyekiti wa UDP.
JK ATUA SHINYANGA KWA STAILI YA PEKEE,AUNGURUMA NDANI YA UWANJA WA KAMBARAGE



helikopta anayotumia JK ikitua nje ya uwanja wa Kambarage na kuamsha msisimko wa aina yake kwa maelfu ya wakaazi wa Shinyanga waliokuwa wakimsubiri kwa hamu Jumatatu hii

Mshike mshike na nguo kuchanika baada ya JK kutua Shinyanga

wana CCM wakimshangilia mwenyekiti wao alipoingia uwanja wa Kambarage, Shinyanga

JK akiingia uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga

JK akipungua wana Shinyanga baada ya kuwasili uwanja wa Kambarage, Shinyanga

JK akihutubia maelfu ya wananchi uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga

JK akimnadi mgombea ubunge wa Shinyanga mjini Bw. S. Masele

Mgombea ubunge Shinyanga mjini Bw. S. Maselew na mai waifu wake baada ya kunadiwa na JK

JK akijichanganya na wana CCM kabla ya kuhutubia maelfu uwanja wa Kambarage

Sehemu tu ya wananchi waliofurika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga

wana CCM wa Shinyanga

Nyomi uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga

Haramia wa Kisomali akamatwa Tanzania

Somalia Flag
Jeshi la Tanzania limesema limemkamata mshukiwa mmoja wa Uharamia raia Somalia, kufuatia makabiliano makali ya ufyatulianaji wa risasi katika bahari ya Hindi.
Ripoti zinasema tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili iliyopita katika eneo la Kusini mwa pwani ya Tanzania, eneo ambalo meli ya kampuni ya kuchimba mafuta ya Ophir inafanya utafiti ili kubainisha ikiwa eneo hilo lina utajiri wa mafuta ya Petroli.
Msemaji wa jeshi la wanamaji nchini Tanzania, Steve Buyuya, amesema manuawari ya kijeshi ilishambuliwa kwa risasi na maharamia waliokuwa kwenye mashua ndogo.
Lakini baada ya ufyatulianaji wa risasi uliodumu kwa muda, maharamia kadhaa walifanikiwa kutoroka huku mmoja wao akikamatwa na wanamaji wake.
Muswada wa Obama wa kudhibitiwa Internet nchini Marekani
Sample Image

Rais Barack Obama wa Marekani anajiandaa kuwasilisha muswada wa kudhibitiwa matumizi ya Intaneti nchini humo.
Kwa mujibu wa muswada huo, maelezo binafsi ya watumiaji wa Intaneti ikiwa ni pamoja na barua-pepe zao na mitandao ya kijamii zitakuwa zinawafikia moja kwa moja polisi wa FBI.
Gazeti la New York Times limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, kama muswada huo utapitishwa, basi maelezo ya wanachama wa mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Skype yatakuwa yanawafikia moja kwa moja polisi wa Marekani FBI itakapobidi.
Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa mbele ya Baraza la Congress la Marekani mwaka ujao wa 2011.
Maafisa usalama wa Marekani wanasema kuwa inabidi sheria na hatua mpya zichukuliwe kwa ajili ya kudhibiti na kuwekea mipaka matumizi na mawasiliano ya Intaneti nchini humo.
Lakini baadhi ya weledi wa mambo wameelezea wasiwasi wao kuwa hatua hizo mpya zitapelekea watu wenye nia mbaya kupenya ndani ya barua-pepe za watu binafsi na kufanya uhalifu na uharibifu. 
Wapalestina watatu wauawa shahidi katika mashambulizi ya Israel
Sample Image

Wapalestina watatu wameuawa shahidi baada ya wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel kufanya mashambulizi katika kambi ya wakimbizi ya al Bureij kusini mwa Ukanda wa Ghaza.
Msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni amedai kuwa Wapalestina hao walikuwa wanajiandaa kurusha maroketi katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni.
Madai kama hayo hutolewa maafisa wa utawala wa Kizayuni kila wanapofanya jinai zao dhidi ya Wapalestina kama njia ya kuhalalisha jinai wanazofanya mara kwa mara katika maeneo ya Wapalestina hasa ya Ukanda wa Ghaza.
Itakumbukwa kuwa kabla ya utawala wa Kizayuni kufanya mashambulizi ya kikatili baina ya mwezi Disemba 2008 na Januari 2009 kwenye Ukanda wa Ghaza, moja ya madai yaliyotolewa na maafisa wa utawala huo dhalimu ili kuhalalisha jinai zao hizo za siku 22 ni eti kulipiza kisasi cha mashambulizi ya maroketi yanayotupwa na Wapalestina kutoka Ukanda wa Ghaza.
Zaidi ya Wapalestina 1,400 waliripotiwa kuuawa shahidi kwenye Ukanda wa Ghaza ambapo ukanda huo ulipata hasara ya zaidi ya dola bilioni 1.6 kutokana na mashambulizi hayo ya siku 22.

Monday, September 27, 2010

Wateja Wa Vodacom Sasa Kuchat Kwa Internet Katika Mitandao Jamii Bure
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Mwamvita Makamba
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imezindua huduma mpya ya Intaneti ambayo itawawezesha wateja wake kuchati kwa intaneti bure.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Mwamvita Makamba alisema jana kwamba wateja wa Vodacom sasa wanaweza kuchati bure kwenye tovuti za Face Book, the Grid na Vodamail.
Alisema Vodacom Tanzania inatoa huduma hiyo kwa lengo la kuwawezesha wateja wake kupata muda wa kuchati zaidi.
Alifafanua kwamba hayo yote yatawezekana kwa kutumia mtandao wa 3G ambao una kasi na nguvu kubwa.
“Tunapenda wateja wetu watumie mtandao wetu kwa kuwasiliana bure na hivyo kukata kiu yao ya mawasiliano”.
Alitoa wito kwa wateja wa Vodacom na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma hiyo ya mtandao wa Intaneti.
Aliwaomba Watanzania kujiunga na Vodacom ili kupata huduma hiyo bure na hivyo kuwasiliana zaidi.
Alisema huduma hiyo itapatikana kwa simu za mkononi na pia kwa Laptop zilizounganishwa na USB Moderm.
Ze Comedy Original wampa Tafu JK
Kundi la kuchana mbavu la Ze Komedi Original likiwasili eneo la tukio wakati wa kampeni za CCM ambapo kundi hili na wasanii wengine nyota kibao wameamua kumpa tafu JK. Hapa ni jimbo la Isimani, Iringa, kwa mgombesa aliyekwishapeta, Mh. William Lukuvi.
Frank Lampard kukosa mechi muhimu
Frank Lampard
Frank Lampard
Frank Lampard atakosa michezo muhimu kwa timu yake ya Chelsea na timu ya taifa ya England kutokana na kuendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa ngiri.
Lampard mwenye umri wa miaka 32 hajaichezea klabu yake kwa mwezi mmoja na meneja wake Carlo Ancelotti amethibitisha kiungo huyo hataweza kucheza kwa takriban wiki mbili zijazo.
Kipindi hicho atakosa mechi dhidi ya Marseille, Arsenal na mchezo wa kufuzu mashindano ya Euro 2012 wakati England itakapopambana na Montenegro.
Ancelotti ameendelea kusema, Lampard hawezi kucheza kwa sasa, wanahitaji muda zaidi tofauti na walivyotazamia.
Kwa vile hajaichezea Chelesea, Ancelotti amesema vile vile hatakuwa tayari kuichezea timu ya taifa.
Lampard alirejea mazoezini baada ya kufanyiwa upasuaji tarehe 31 mwezi wa Agosti, lakini amekuwa akisumbuliwa na maumivu kwenye kovu.
Tayari amekosa mechi za England walizoshinda za kufuzu michezo ya Euro 2012 dhidi ya Bulgaria na Switzerland mapema mwezi wa Septemba na pia atakosa mechi dhidi ya Montenegro katika uwanja wa Wembley tarehe 12 mwezi wa Oktoba.
Mara ya mwisho kuichezea Chelsea ilikuwa tarehe 28 mwezi wa Agosti timu hiyo ilipoifunga Stoke mabao 
2-0.

Saturday, September 25, 2010

Watu wengi duniani wanakubaliana na hoja za Rais Ahmadinejad kuhusu tukio la Sept 11

Sample Image
Siku ya Alhamisi Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliuambia ulimwengu kuwa tukio la Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani bado lina utata na hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa lilikuwa shambulizi la kigaidi. Tamko hilo la Rais wa Iran lililowakasirisha mno watawala wa Washington limepata uungaji mkono kutoka kila pembe ya dunia. Katika miaka ya huko nyuma tafiti mbali mbali zilionyesha kuwa watu wengi wanaamini kuwa Marekani na Utawala haramu wa Israel kwa pamoja zilishirikiana katika kupanga tukio hilo. Nchini Jordan asilimia 31 ya wananchi wanaamini kuwa tukio hilo lilifanyika ima kwa msaada wa Marekani au kwa ridhaa yake na nchini Misri asilimia 46 pia wanaamini hivyo. Mrekani kwenyewe uchunguzi wa maoni wa mwaka 2006 uliofanywa na shirika la Scrippsnews ulifichua kuwa asilimia 36 ya Wamarekani wanaamini kuwa serikali yao ilihusika kwa njia moja au nyingine katika utekelezaji wa tukio hilo. Rais Mahmoud Ahmadinejad ametoa changamoto kwa Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi huru kuhusu tukio hilo.

Mugabe: Mataifa 2 ya Afrika yaongezwe katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Sample Image
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametoa wito wa kuongezewa mataifa mawili ya barani Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC. Akizungumza katika kongamano kuu la Umoja wa Mataifa hapo jana mjini New York Marekani, Rais Mugabe amesema, mataifa hayo yanafaa kujumuishwa kama wanachama wa kudumu wa baraza hilo na kupewa haki ya veto ili kuwa sauti itakayoyawezesha kupaza changamoto zinazozikabili nchi za bara hilo. Mugabe amekosoa sera na kanuni zinazoendesha baraza hilo na kutaka zifanyiwe marekebisho au zibadilishwe. Aidha, ameyataka mataifa yanayotajwa kuwa yenye uwezo mkubwa duniani yakomeshe unafiki wao wa kuhubiri demokrasia huku yakifeli kutekeleza ahadi zao. 




MTANDAO WA JK

Kwa habai na picha za kampeni mgombea urais wa CCM, tembelea hapo chini:

Friday, September 24, 2010

MKUTANO WA KUHAMASISHA WAISLAM KWENDA HIJJA

Na Mary Kweka - Maelezo.
Taasisi ya kiislam ya Tanzania Hajj Mission ikishirikiana na ubalozi wa Iran Inchini imeandaa mkutano wa kimataifa utakaofanyika Jijin Dar es salaa, wenye lengo la kutoa semina ya Hijja na umoja wa Umma wa Kimataifa wa Kiislam na kuwahamasiha waislamu kujua masuala mbalimbali yahusuyo Ibada ya Hijja.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa taasisi hiyo Shekhe Khalid Mohammed Mrisho wakati akizungumza na wandishi wa habari juu mkutano huo utafanyika tarehe 26 hadi 27 mwezi huu jijini Dares salaam.
Alisema kuwa mkutano huo unalenga kuhamasisha Idadi ya Watanzania wengi kushiriki Ibada ya Hijja ili kutimiza idadi rasmi iliyotolewa na Serikali ya Saudi Arabia.
“Watanzania wanaoenda Hijja kila mwaka hawazidi 2000 wakati nafasi tunayokuwa tumeandaliwa na serikali ya Saudi Arabia ni watu 30,000, hivyo tumeona upo umuhimu wa kuwahamasha waislamu wa Wa tanzania kijitokeza kwa wingi japo kufikia 2500 mwaka huu”.
Akizitaja mada zitakazoongelewa kwenye majadala huo , Shekhe Khalid Mohammed amesema ni Kumkumbuka Allah(swt)katika Hijja na Faida nyingine za Hijja, Falsafa ya Hijja, Hijja na kisimamo cha watu,Hijja na haki za binadam duniani na Hadhi ya mwanamke na Sayyida Hajar katika Hijja.
Zingine alizozitaja ni Uwezo wa utekelezaji waa Ibada ya Hijja katika Afrika, Taratibu za Hijja na wananyokubaliana baina ya Sunni na Shia,Hijja na Siasa, Fursa na vikwazo vya Hijja katiak Afrika na kuunda Utamaduni wa hamu ay Hijja miongoni mwa waislam wa Afrika .
Aidha Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa Mkutano huo pia utahamasisha kujenga umoja wa kimataifa wa Umma wa Kiislam kwa Tanzania na nchi zingine za kiislam duniani.
Kwa upande wa Balozi wa Iran inchin Bwana Mohsen Movahhed Ghomi amesema Serikali ya Irani inashirikiana na Tasisi ya Tanzania Hajj Mission kuhakikisha Waislamu wa Tanzania wanapata uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa kwenda Hijja na kujitokeza kwa wingi kufanya Ibada hiyo kila mwak
Ibada hii ya hijja, ni moja kati ya nguzo tano za Uislam na kwamba wanaopaswa kuitekeleza ni wale wenye uwezo na kwa wale wasiokuwa nao hawalazimishwi kuhiji, ni Ibda inayofanyika kwa waislamu kutembelea sehemu tukufu za Saudia Arabia na Mecca na hufanyika kila mwaka .

Mwenye matatizo ya akili anyongwa nchini Marekani


Sample Image
Teresa Lewis mwanamke mwenye umri wa miaka 41 mwenye matatizo ya akili amenyongwa leo nchini Marekani kwenye jimbo la Virginia, kwa kosa la kumuua mumewe na mjukuu wake wa Kambo. 
Teresa ni mwanamke wa kwanza kuhukumiwa adhabu ya kifo nchini Marekani tangu mwaka 1912 na amesubiri kutekelezewa adhabu hiyo kwa muda wa miaka mitano. 
Mwanamke huyo ameuawa kwa kudungwa sindano ya sumu. Maswali mengi yamejitokeza kuhusiana na uwezekano wa mama huyo aliyekuwa na kiwango cha akili cha IQ 72 kupanga na kutekeleza mauaji hayo ya watu wawili, ambaye pia imejulikana alikuwa na matatizo ya akili. 
Mahakama kuu ya Marekani na Gavana wa jimbo la Virginia walikataa kuondoa adhabu hiyo ingawa wengi wametilia shaka kesi hiyo na maelfu ya watu walitaka iondolewe. Virginia ni jimbo la pili nchini Marekani linaloongoza katika utendaji vitendo vya jinai. 

Mahakama ya Kenya yawapata na hatia ya uharamia Wasomali 7

Sample Image
Mahakama ya Mombasa nchini Kenya imewapata na hatia ya kufanya uharamia Wasomalia 7 na kuwahukumu kifungo cha miaka mitano jela kwa kuteka nyara meli ya Uhispania mwaka 2009. Wasomalia hao wamehukumiwa baada ya kutiwa mbaroni mwezi Mei mwaka uliopita. Suala la kuwahukumu maharamia wa Kisomali wanaokamatwa limekuwa likikwamishwa na kuzusha hitilifau za mitazamo juu ya nchi gani wahukumiwe maharamaia hao. Somalia yenyewe haina vyombo vya sheria vya kuendesha kesi hizo. Kenya ina wasiwasi kuwa maharamia wanaoachiliwa baada ya kutumikia vifungo vyao jela na wale wasiopatikana na hatia watalundikana nchini humo, na suala hilo kuhatarisha usalama wa nchi hiyo. Kuna maharamia wa Kisomali 15 wanaotumikia kifungo nchini Kenya huku mamia ya wengine bado wakiwa wanaendelea kushikiliwa. 

Obama ashinikiza kura ya haki Sudan


Rais wa Sudan Omar al-Bashir

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuhudhuria mkutano maalum wa Umoja wa Mataifa kushinikiza maafisa wa Sudan kuhakikisha kura ya maoni ya mwezi Januari iwe huru na ya haki.
Sudan Kusini inatarajiwa kupiga kura ya kuamua iwapo eneo hilo lijitawale lenyewe au la.
Lakini maandalizi yanaonekana bado hayajakamilika, huku serikali mpaka sasa ikiwa haijaamua nani wa kupiga kura.
Upande wa Kusini unasisitiza kura hiyo ipigwe kwa wakati uliopangwa, na usiahirishwe.
Kura hiyo ya maoni ni sehemu ya makubaliano ya amani ya mwaka 2005 ya kumaliza miongo miwili ya mapigano baina ya upande wa kaskazini na upande wa kusini wenye utajiri wa mafuta, lakini waangalizi wanahofia ucheleweshaji au ukosefu wa kura zenye kuaminika unaweza kuchochea mgogoro upya.
'Hatari ya kulipuka'

Slav Kiir
Mwandishi wa BBC James Copnall aliyopo mjini Khartoum alisema kunahitajika azma ya kweli ya kisiasa, vile vile vifaa vya kutosha, ili kuweza kupiga kura hiyo kwa muda unaotakiwa - lakini mpaka sasa, vyote hivyo havipo.
Mwandishi wetu alisema, huu ni mkutano wa Umoja wa Mataifa, lakini bila ya shaka kuwepo kwa Bw Obama ni muhimu.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir amerudia mara kwa mara akisema kura hiyo itakuwa huru na ya haki, lakini wakosoaji hawaamini, na baadhi wanamshutumu kwa kuisogeza mbele kusudi.
Bw Bashir, anayetakiwa na umoja huo kwa makosa ya uhalifu wa kivita, anawakilishwa na makamu wake Ali Osman Taha, huku Sudan Kusini ikiwakilishwa na kiongozi wake Salva Kiir.
Mapema mwezi huu, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton aliita kura hiyo ya Januari 9 "bomu linalokaribia kulipuka'.
Alionyesha wasiwasi kuwa upande wa kaskazini si rahisi kukubali kupoteza nafasi yake ya kugawana mapato ya mafuta na upande wa kaskazini ujitahidi kuwapa nafasi hiyo, ili kuzuia mapigano kujirudia.
Sudan Kusini, ambapo wengi ni Wakristo au hufuata imani za kiutamaduni, tayari inajitawala kwa kiasi fulani na inaongozwa na waliokuwa waasi wa SPLA, waliopigana na wengi ambao ni waislamu, wanaozungumza kiarabu upande wa kaskazini mpaka makubaliano yalipofikiwa mwaka 2005

Thursday, September 23, 2010


***HAPPY BIRTHDAY BELY KASAMBULA KEMA  ***

BELY KASAMBULA KEMA
LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MDAU WA BLOG HII KAKA BELY KASAMBULA KEMA  WA DAR ES SALAAM TANZANIA.
BLOG HII INAUNGANA NA FAMILIA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KUMTAKIA KILA LA HERI KATIKA SIKU YAKE HII YA KUZALIWA.
MOLA AKUPE AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU,BUSARA NA HEKIMA  KATIKA MAISHA YAKO.
Happy Birthday!
HAPPY BIRTHDAY KAKA 

BELY KASAMBULA KEMA.



Dk Slaa Atia Fora Moshi...
Mapokezi makubwa kwa mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chadema Dr.Willibrod
Slaa jana mjini Moshi Kilimanjaro
Mgombea ubunge wa jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, akiwahutubi maelfu ya wakazi wa mji wa Moshi, waliojitokeza katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa jana
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (.CHADEMA), Freeman Mbowe, akiwaongoza maelfu ya wakazi wa mji wa Moshi kulia kilio cha umasikini, wakati alipohutubia mkutano wa kampeni za mgombea wa urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa jana.
Picha zote na Joseph Senga.

Zitto Kabwe Amnadi Mgombea Wa Chadema Mtwara Mjini
Zitto kabwe akimwaga sera mtwara mjini
Mgombea wa Chadema Mtwara Mjini-Ndugu Athman Jetha Edwin


Zitto kabwe (kushoto)mgombea wetu wa Mtwara Mjini-Ndugu Athman Jetha Edwin
Sehemu ya umati wa watu ukiwa umemzunguka zitto kabwe
Sehemu ya umati mkubwa uliyojitokeza kumsikiliza zitto kabwe kwenye kampeni za kumnadi mgombea ubunge mtwara mjini kwa tiketi ya cha cha chadema athman jeth edwin.
Na haki-hakingowi.blogspot.com

Redio ya Somalia yaisusia Hizbul Islam

Waandishi wa habari kutoka Somalia wameisusia redio moja iliyotekwa hivi karibuni na wapiganaji katika mji mkuu Mogadishu.
Wafanyakazi katika kituo cha redio cha GBC walikataa kupokea amri kutoka kundi la wapiganaji la Hizbul Islam, kwani ilikuwa inaingilia uhuru wa kujieleza.
Awali, Hizbul Islam iliruhusu redio binafsi kufanya shughuli zao kwenye eneo lao, ila tu walizuia kupiga muziki, ambao husema ni kinyume na Uislamu.
Mpiganaji wa Hizbul Islam
Wakati huo huo, kumekuwa na mapigano makali katika mji mkuu kabla ya kuwepo mkutano wa kujadili mgogoro wa Somalia kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa. Katibu mkuu wa umoja huo Ban Ki-moon aliuitisha mkutano huo mjini New York kujadili mgogoro wa kisiasa na kiusalama unaoongezeka. Mapema wiki hii, waziri mkuu alijiuzulu kutoka serikali hiyo dhaifu inayoungwa mkono na umoja wa mataifa inayoongozwa na Muislamu mwenye msimamo wa kati Rais Sheikh Sharif Ahmed. Serikali hiyo, inayoungwa mkono na wanajeshi 6,000 wa Umoja wa Afrika, inadhibiti eneo dogo tu la mji mkuu wa nchi hiyo. Mwandishi wa BBC Mohammed Olad Hassan mjini humo alisema watu 19 wameuawa katika mapigano yaliyoanza siku ya Alhamis asubuhi. Takriban watu 68 wamejeruhiwa wakati majeshi ya serikali, yanayoungwa mkono na majeshi ya Umoja wa Afrika, yakipambana na wapiganaji kaskazini na kusini mwa Mogadishu. Kumekuwa pia na urushaji wa makombora katika soko la Barkara. Waandishi wanasema vituo vya redio vinatoa taarifa muhimu sana kwa wakazi wa Mogadishu, wanaohitaji kutwa kujua ni maeneo gani hayako salama. Hizbul Islam na kundi la al-Shabab hudhibiti eneo kubwa la Somalia ya kati na kusini.

Titus Bramble atuhumiwa kumbaka mwanamke


Titus Bramble
Mlinzi wa Sunderland Titus Bramble, amekamatwa baada ya mwanamke kubakwa kwenye hoteli moja mjini Newcastle.
Mchezaji huyo wa Ligi Kuu ya England amekamatwa pamoja na mtu mwengine katika hoteli ya Vermont mapema siku ya Jumatano na wanahojiwa na polisi.
Bramble mwenye umri wa miaka 29 amekamatwa kwa kushukiwa amebaka baada ya polisi kupigiwa simu na mwanamke mmoja.
Klabu ya Sunderland hadi sasa haijazungumza lolote kuhusiana na tuhuma hizo. Bramble alijiunga na klabu hiyo akitokea Wigan msimu huu.
Msemaji wa kituo cha polisi cha Northumbria, amesema wanaume wawili, wakiwa na umri wa miaka 29 na 30 wamekamatwa wakituhumiwa kubaka mwanamke.
Bramble pia aliwahi kuichezea New Castle na Ipswich.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUSOMA HABARI ZILIZOPITA BOFYA NENO OLDER POSTS HAPO JUU ASANTE SANA KWA KUTEMBELEA NA KARIBU TENA