
Tendulkar anasemekana kuwa mchezaji bora zaidi wa kriketi duniani...lakini hiyo ni hoja inayoendelea kujadiliwa
Amepewa jina la 'maximum city' na mwandishi vitabu maarufu sana, huku mji wa Mumbai ukimuaga mchezaji kriketi mashuhuri zaidi nchini India.
Mchezaji bora zaidi wa Kriketi nchini India hii leo, ameondoka rasmi katika ukumbi wa mchezo huo, katika kile kinachosemekana kuwa mchezo wa lala salama wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40, India itamenyana na West Indies katika mchuano wa mwisho wa Test katika uwanja mashuhuri wa Wankhede.



