
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa maktaba ya Shule ya Msingi ya Mzimuni iliyoko Magomeni. Kushoto kwa Mama Salma ni Mheshimiwa Balozi Young-Shim Dho, Mwanzilishi wa Step Foundation na Balozi wa Mradi wa Utalii endelevu kwa ajili ya kuondoa umasikini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani ambaye ndiye aliyefadhili maktaba hiyo.



