TIMU
ya taifa ya Libya imetwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2014
baada ya kuifunga Ghana kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana
Jumamosi Uwanja wa Cape Town.
Ushindi huo ni sawa na Libya kulipa kisasi kwa Ghana baada ya kufungwa kwa penalti 7-6 miaka 32 iiliyopita kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).



