skip to main | skip to sidebar SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Pages

  • Home
  • ABOUT
  • SPORTS
  • ADVERTISEMENT
  • WEBSITES
  • CHAT ROOM
  • TV
  • RADIO
  • CONTACT

Allyshams Blog

24 SEVEN 365 "HARAKATI HAZIKOMI"

Thursday, February 11, 2016

CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU IRINGA (IRFA) KUJENGA UWANJA WA KISASA

kulia  ni mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu  mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na baadhi ya viongozi wa uwanja wa samora.
NA FREDY MGUNDA
IRINGA
Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa (IRFA) kiko mbioni kujenga uwanja wake wa kisasa utakaosaidia kuendeshea ligi mbalimbali zikiwemo ligi za kimataifa  hali itakayosaidia  kuinua soka la mkoa huo .

Akizungumza ofisini kwake mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu  mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava alisema wameamua kujenga uwanja wao  ili kuepukana na adha wanayopata kutokana na kukosa sehemu ya kuendeshea ligi  mbalimbali .

Alisema tayari wameshapata eneo la hekari 14 katika eneo la kitwiru ndani ya manispaa ya Iringa  na sasa kinachosubiriwa ni kumaliza mazungumzo kati ya chama hicho na manispa ya Iringa ili kuweza kumilikishwa eneo hilo ili liwe mali yao kabisa tofauti na apo awali ambao manispaa hiyo ilikuwa inataka kuingia nao ubia

“Tayari hili swala liko katika hatua za mwisho na tayari tumesha fanya mazungumzo tunataka  tujenge  uwanja wetu wenyewe wa kisasa ambao tunaweza kucheza mechi za kimataifa  kwani tumekuwa tukipata tabu ya viwanja vya kuchezea na hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuuwa soka la mkoa wetu ”alisema Kuyava

Alisema wanasubiri majibu ya maombi waliyopeleka katika manispaa hiyo ili kuweza kupunguziwa bei li kuanza mchakato wa kulipa fidia kwa wamiliki wa maeneo hayo ili waanze mchakato wa uwanja huo wa kisasa .

Alisema kuwa mara nyingi timu zimekuwa hazi pati kitu  wanapotumia viwanja vya watu  kwani asilimia 16 za mapato yanayopatikana kutokana na kingilio huchukuliwa na wamilika  wa kiwanja na asilimia ndogo inabaki ndio zinagawanywa katika maeno mengine na kujikuta timu hazinufaiki na chochote .

Alisema kuwa hapo awali walikuwa wakitumia uwanja wa samora ambao bado uko katika matengenezo tena ya kusuasu kwa kuwa mpaka sasa bado wanadai kusubiri nyasi za kupanda jambo litakalorudisha michezo nyuma endapo hawatakuwa na maono ya kuwa na kiwanja chao wenyewe .

Kwa upande wa wadau wa soka mkoa wa Iringa Ally salehe ambaye pia ni shabiki wa timu ya lipuli anasema kuwa endapo juhudi za makusudi zitafanyika na kufanikisha ujenzi wa uwanja huo basi ni dhahiri kuwa soka la mkoa wa iringa litapanda  kwa kiasi kikubwa .

Alisema kuwa katika mkoa wa Iringa kuna vipaji vingi vya michezo  ikiwemo wachezaji wa mpira wa miguu lakini wamekuwa wakikosa sehemu za kufanyia mazoezi ili kukuza vipaji vyao  hivyo kujengwa kwa uwanja huo wa kisasa utafungua fursa za ajira kwa vijana wengi.

Posted by Ally Shaaban Mgido's at Thursday, February 11, 2016 Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook

0 comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014

BOFYA HAPA KUONA MATOKEO HAYO

Translate this Blog

English French German Spain Italian Dutch Russian Portuguese Japanese Korean Arabic Chinese Simplified

About Me

My Photo
Ally Shaaban Mgido's
Dar es salaam, Tanzania
Phone: 0755993639, 0657615174
E-mail: ally.shaaban@yahoo.com
View my complete profile

Followers

Blog Archive

LIVE TRAFIC FEEDS

"TANGAZO: UNAHITAJI BIDHAA ZA UREMBO WASILIANA NASI HAPA"

Copyright © 2009 Allyshams Blog All Rights Reserved. | Modified & Development by 24 SEVEN 365.. Powered by Blogger.

Total Pageviews

TANGAZA BIASHARA YAKO NASI HAPA

TANGAZA BIASHARA YAKO NASI HAPA

Popular Posts

  • Matokeo Ya Mtihani Wa Darasa La Saba 2013
  • Do you feel you don’t have the time or money to give to your children all you would like?
  • KIFO CHA WHITNEY HOUSTON BOBY BROWN AHUSISHWA
  • ASKARI WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI DOGO JANA SAA SITA USIKU.
  • (no title)
  • The Most beautiful Business in the World explained in swahili language.
  • Are you like Me 8 years AGO?
  • Amani Millanga:Vijana na Maandamano, Polisi na Mauwaji: Tunaelekea Wapi?
  • PRESIDENT KIKWETE AWARDED HONORARY PROFESSORSHIP BY CHINA AGRICULTURAL UNIVERSITY
  • Yemen Celebrates As President Steps Down

WANAOTEMBELEA


WEBSITES & BLOGS

  • Allyshams
  • Amazingnetmark
  • Myummah76
  • Francis Godwin
  • Globalpublishers
  • Full Shangwe
  • Ladyjaydee
  • Swahili TV
  • TMF
  • Haki Ngowi
  • Mimi na Tanzania
  • Mo Blog
  • Chadema Blog
  • CCM Blog
  • January Makamba
  • Zitto kabwe
  • Habari Leo
  • Daily News
  • Mwananchi
  • Mtanzania
  • Tanzania Daima
  • Raia Mwema
  • Majira
  • Mwanaspoti
  • The Citizen
  • Daraja Letu
  • IPP Media
  • Bashir Nkoromo
  • BBC Swahili
  • Sauti ya Amerika
  • Jamii Forums
  • Michuzi
  • Jiachie
  • BongoBlogs
  • Wavuti
  • SIKILIZA KWANZAJAMII RADIO


    JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

    JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

    SIKILIZA CLOUDS RADIO

    MATOKEO YA KIDATO CHA NNE(IV) SOMA HAPA

    MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2013

    MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2013

    Siasa

    SIKILIZA NYIMBO MPYA



    UNATAKA KUPUNGUA UZITO!!


    CLICK THIS IMAGE

    Contact Form

    Name

    Email *

    Message *

    Allyshams Blog

    24 SEVEN 365 "HARAKATI HAZIKOMI"

    Habari za Nyumbani

     
    Copyright (c) 2011 Allyshams Blog. Developed by ALLY S. MGIDO +255657615174 | +255783149561