
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unapenda kuwatangazia wadau wake na
wananchi wote kwa ujumla kuwa umebadili muda wa saa za kazi kwa ofisi
zake kote nchini. Mabadiliko haya yanatokana na ukweli kwamba wadau wa
Mfuko wanawahi sana kufika ofisi za Mfuko kupata huduma. (Uzoefu wa
Mfuko unaonyesha wadau hufika kabla ya saa 2 asubuhi kupata huduma).
Hivyo,
kuanzia tarehe 1 Agosti 2014 ofisi za NHIF zitakuwa wazi kuanzia saa
moja na nusu (1.30) asubuhi hadi saa kumi kamili (10:00) jioni kuanzia
Jumatatu hadi Ijumaa.
Huduma zote zinazotolewa
na Mfuko zitaendela kutolewa kama kawaida muda huo na wote mnakaribishwa
kuendelea kupata huduma za Mfuko kama kawaida.
NHIF: "Huduma bora za matiabau ni haki yako na ni dhamana yetu"
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Kaimu Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,
S.L.P.11360, Dar es Salaam; Simu: 022 2133969/964;
Barua pepe: info@nhif.or.tz; Tovuti: www.nhif.or.tz




0 comments:
Post a Comment