Chai ni kinywaji maarufu sana nchini India. Nchi hiyo hutumia tani
837,000 za chai kila mwaka. Unywaji wa Chai una dalili zake kila mahali
hata katika mitaa na barabara za India. Watu wanaopakua Chai
wanajulikana kama Chai Wallah ambao huiweka viungo, sukari na maziwa
Lalu Yadav ameshuhudia maelfu ya miili ya watu ikichomwa kama ulivyo
utamaduni wa wahindi kuchoma miili ya wafu. Kibanda chake kiko karibu na
eneo la maziko na sehemu ya kuchomea maiti
Ganesh, ambaye ni Chai Wallah, huuzia chai yake katika kituo cha treni
katika jimbo la Bihar. Hapa anapika chai yake ya mwisho leo. Watu wengi
nchini India huhusisha Chai na usafiri wa treni.
Kibanda hiki cha kuuza Chai ni chake Shobhan Barwa , kipo katika mtaa wa
kifahari mjini Calcutta. Yeye hupata wateja wengi wakati wa tamasha la
kihindi lijulikanalo kama Durga Puja
Santon anachunga Chai ambayo huiuza katika duka lake mjini Mumbai.
Alianza kuuza Chai miaka 15 iliyopita na eneo analouzia Chai hiyo
limebadilika sana.
Picha hizi zimepigwa na wapigapicha Resham Gellatly na Zach Marks.
Unaweza kuona picha zao nyingine kwenye blogu yao
CHANZO: BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment