NDEGE
zilizobeba miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya ndege ya
Malaysia MH17 zimeondoka kutoka Ukraine kuelekea nchini Uholanzi kwa
ajili ya kutambuliwa.
Katika ajali hiyo iliyotokea Julai 17 mwaka huu, jumla ya watu 298 walipoteza maisha huku 193 wakiwa raia wa Uholanzi.
Maofisa
wa Uholanzi wanadai kupokea jumla ya miili 200 kutoka kwa wapiganaji
wanaoiunga mkono Urusi japo wapiganaji hao wanadai kupakia miili
iliyokamilika 282 na viungo vya miili 16 katika treni iliyopeleka miili
hiyo eneo lililo chini ya serikali ya Ukraine huko Kharkiv.




0 comments:
Post a Comment