SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, May 8, 2014

Wito wa kuwaokoa wasichana Nigeria

Kofi Annan aomba mataifa Afrika kuja pamoja

Viongozi kumi na watatu wa mataifa na mamia ya wafanyabiashara wanakutana Abuja kwa mkutano wa biashara na masuala ya uchumi duniani kuhusu Afrika.

Mkutano huo mwaka huu ulikuwa ni fursa kwa Nigeria baada ya kutajwa kuwa nchi yenye uchumi mkubwa Afrika, lakini mashambulio ya kundi la wapiganaji wa Boko Haram na wasiwasi wa kiusalama yameugubika mkutano huo.
Hisia mbali mbali zimemiminika kufuatia mashambulio yanayoendelea nchini Nigeria.
Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan, ametoa wito wa hatua kuchukuliwa dhidi ya mashambulio hayo, na ameishutumu serikali ya Nigeria na mataifa ya Afrika kwa kutochukua hatua haraka kufuatia utekaji nyara wa wasichana wa shule takriban 200 nchini humo.
Annan ameyaomba mataifa hayo kutumia walichonacho kusaidia kuwaokoa wasichana hao.
Alisema, 'Nadhani Afrika ingekuja pamoja na kulaani kwa harama kitendo hicho na serikali ya Nigeria nayo ingewafariji ummma kwa kueleza kwa uwazi juhudi wanazofanya kuwatafuta na kuwaokoa wsichana hao'.
Msichana wa Pakistani aliyeponea kupigwa risasi na wapiganaji wa kundi la Taliban, Malala Yousafzai, amesema, 'Wanayofanya ni kinyume kabisa na dini -nawashauri waisome na kuifuata koran - koran inatoa ujumbe wa amani, utu na uadilifu. Kilichofanyika kweli kinanihuzunisha'.
Malala ameeleza kwamba dunia haipaswi kunyamaza kuhusu utekaji wa wasichana hao takriban 200 Nigeria.