SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, April 17, 2014

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Wanaounga Mkono Mfumo wa Serikali Tatu Wakisusa na Kutoka Nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Jioni Jana


Wajumbe wa Bunge  Maalum la Katiba ambao wanaounga mkono mfumo wa  Serikali za tatu wakitoka katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikao.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO
-----
WAJUMBE karibu wote wa vyama vya upinzani wanaoshiriki Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, wametoka nje ya kikao cha leo jioni, wakipinga kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye wajumbe wengi ndani ya bunge hilo, kuwaburuza.

Wakati akitoa mchango wake, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliliambia Bunge kuwa wanashangazwa na kitendo cha CCM kutaka kutumia wingi wao, kutengeneza katiba ambayo hailingani na mawazo ya wananchi, kama yalivyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.

Alisema kitendo kilichofanywa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, kwenda katika kanisa na kusema wanaotaka muundo wa serikali tatu wanataka kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kiislamu ni uchochezi unaoweza kuligawa taifa na hata kusababisha machafuko.

Alisema pia wanashangazwa na Rais Kikwete kupokea na kusaini rasimu hiyo, lakini akaja bungeni na kuipinga kwa nguvu kubwa.