Helikopta
waliyokua wakisafiria Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal, waziri wa ujenzi
John Magufuli, Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman
Kova na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick imepata ajali
asubuhi wakati ikipaa kutoka uwanja wa ndege Dar es salaam. (kwa mujibu
wa mashuhuda)
Taarifa
zilizotoka muda mfupi baadae zimeeleza kupata majeruhi lakini hakuna
yeyote aliepoteza maisha baada ya Helikopta hiyo kuanguka wakati ikianza
safari kuwapeleka viongozi hao kutembelea maeneo yaliyoathirika na
mafuriko.
Wote
walitoka salama na majeraha madogomadogo ambapo pia kwenye taarifa
nyingine iliyotolewa na TBC, wameendelea na ziara ya kutazama athari za
maafuriko kwenye sehemu mbalimbali ikiwemo Pwani.
Ajali hii ya
Helikopta imetokea siku moja baada ya ndege ya shirika la ndege la Kenya
kubamiza chini na kuharibu upande wa kulia wa bawa kutokana na ukungu
mkubwa uliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam wakati ikitua
kutokea Nairobi, hakuna aliepoteza maisha ila waliojeruhiwa wakati wa
kushuka kwa dharura kutoka kwenye ndege.
Taarifa kutoka
kwa mmoja wa Waliokuwemo kwenye Helikopta hii ya jeshi inasema wakati
inapaa kwenye umbali wa kama futi tano hivi kutoka uwanja wa ndege Dar
es salaam, ilizidiwa na upepo ulioirudisha nyuma na kuangukia paa kabla
ya kutua chini.
Kilichofanyika
ni watu waliokuwemo kutoka nje harakaharaka kisha aliekua akiiendesha
kufungua tenki la mafuta na kumwaga mafuta yote alafu baada ya muda
mfupi vikosi vya zimamoto vikaanza kuipiga maji helikopta hiyo ili
kuepusha mlipuko.
Unaambiwa
kama ingekua ni majira ya moto, helikopta hii ambayo ilikua inawapeleka
kutazama maafuriko yaliyookana na mvua Dar es salaam ingeweza kuwa
kwenye hatari zaidi ya kulipuka.
Picha zote mbili kutoka http://nasmamafoto.blogspot.com/